Masomo Yaliyofundishwa Mtandaoni na Taasisi ya Elimu 12/05

Mathematics-The Number System Quadrilateral

 ENGLISH LISTENING SKILLS PROBLEM SOLVING PART A

Masomo mapya yanawekwa katika ukurasa huu kila siku. Kuona masomo yaliyopita, mengi zaidi, ingia katika channel ya Taasisi ya Elimu huko YouTube.

Kufuatia shule kufungwa nchini kwa sababu ya ugonjwa wa Korona, Taasisi ya elimu imeamua kutoa masomo kwa njia ya mtandao ili kuweza kuwasaidia wanafunzi wote nchini Tanzania.

Nchini Tanzania, madarasa yanayotegemea kufanya mtihani mwaka huu ni: darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita. Hata hivyo, masomo hayatolewi kwa vidato vinavyofanya mtihani pekee, bali yanatolewa kwa vidato vyote.

Masomo yanatolewa kwa kutumia televisheni na mtandao. Bila shaka mpango huu utawafaa sana wanafunzi ambao wako nyumbani kufuatia kufungwa kwa shule.

Wanafunzi wawapo nyumbani, wazingatie ushauri wangu huu:

Kwanza, wajilinde na ugonjwa wa korona kwa kufuata ushauri wa wataalamu ikiwemo: kunawa kwa maji tiririka na sabuni, kutumia vitakasa mikono, kuepuka mikusanyiko na kanuni nyinginezo.

Pili, wajisomee, mwanafunzi anashauriwa afuate ratiba ileile aliyokuwa nayo shule. kama ulikuwa unaingia darasani saa mbili asubuhi, basi hapohapo nyumbani anza kujisomea saa mbili asubuhi. Kama muda wa mapumziko ilikuwa saa nne asubuhi, nawe pumzika saa nne asubuhi. Kwa kifupi ni kwamba, fuata ratiba ya shule ukiwa hapohapo nyumbani.

Jambo la tatu, wanafunzi wasiwe na hofu. Hata kama upo kidato cha mtihani, amini kwamba, kufungwa kwa shule siyo sababu ya wewe kufanya vibaya katika masomo yako. Utafanya vizuri, muhimu ni kuutumia vizuri muda huu ukiwa nyumbani.

Kanuni za kufaulu mitihani yako bado zipo palepale: kanuni ya kwanza ni kufundishwa, masomo yanafundishwa kwa njia ya mtandao.

Kanuni ya pili ni kujisomea, tayari nimesisitiza uutumie muda wako vizuri hapo nyumbani kwa kujisomea.

Kanuni ya tatu ni kufanya maswali ya mwalimu, katika masomo maswali yanatolewa, hivyo fanya maswali hayo.

Kanuni ya nne ni kufanya mitihani ya mwalimu, ipo mitihani mingi online unaweza ukafanya kadri unavyotaka.

Kanuni ya tano ni kupitia mitihani iliyopita, ipo mitandao mingi ina mitihani iliyopita, tembelea mitandao hiyo kujipatia nakala ya mitihani iliyopita.

Kanuni ya sita ni kusoma notes au vitabu sahihi, natumaini una notes na vitabu sahihi kama huna tafuta sasa.

Kanuni ya mwisho ni kuzingatia muda, hii nimeisisitiza mwanzoni kuwa unatakiwa kuzingatia muda uwapo nyumbani wakati huu. Ratiba ya shule, ihamishie nyumbani.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie