Tabia Nzuri Zinazosaidia Kukamilisha Mipango Mbalimbali
Mipango
lazima ikamilike. Lakini inawezekana mipango yako haikamiliki kwa sababu
umekosa tabia hizi ninazokufundisha leo:
1.
Amka
muda unaofanana kila siku
Wikendi,
sikukuu na siku ya kuzaliwa zikiwemo. Bila kujali umelala saa ngapi leo, amka
muda uleule siku zote. Kama unaamka saa 12 asubuhi, basi iwe hivyo kila siku. Kama
unaamka saa mbili asubuhi, iwe hivyo.
2.
Soma
vitabu
Vitabu
vitakufanya ujifunze mambo mbalimbali. Maarifa mengi yamefichwa vitabuni,
usiache kuyapata.
3.
Tafakari
siku yako
Fikiria
siku iliyopita umefanya nini, pia fikiria siku ya leo utafanya nini na siku ya
kesho utafanya kitu gani. Weka mipango ya siku ijayo na ikumbuke siku
iliyopita.
4.
Orodhesha
mambo ya kufanya kwa siku husika
Orodhesha
mambo unayotakiwa kufanya katika siku husika. Kama siku hiyo umepanga kuangalia
filamu, kuchat na marafiki, kusoma kitabu na kwenda kufanya mazoezi andika. Ukiandika
itakusaidia kufanya kazi kwa utulivu bila kutafakari ni kitu gani kingefuata
baada ya kazi uliyonayo kukamilika.
5.
Zungumza
na mtu anayekuzidi katika kitu fulani
Mara
mojamoja, jaribu kukaa na watu wanaokuzidi katika mambo fulani. Kama ni mwanafunzi,
kaa na wanafunzi wenzako wanaofanya vizuri zaidi. Kama ni mfanyabiashara, kaa
na mtu anayefanya biashara vizuri kukuzidi, muhimu kuwa na mtu ambaye ni bora
katika jambo fulani. Kuwa naye kutakufanya ujifunze vitu vingi kutoka kwake.
6.
Cheka
angalau mara moja kwa siku
Tazama
video za kuchekesha, tazama vituko vya mtandaoni, na unapokuwa peke yako, kuwa
kama mtoto. Jitahidi ucheke mara nyingi uwezavyo kwa siku, lakini kama mara
nyingi haiwezekani, basi cheka angalau mara moja. Nakukumbusha kuwa, ni rahisi
kucheka kuliko kulia!