Mambo Muhimu ya Kumfundisha Mtoto Yeyote

Mwanasesere.
1.   Watu wakikuuliza unataka kuwa nani ukiwa mkubwa, wajibu huna mpango wa kuwa mkubwa
Waambie utaamua ukikua. Waeleze kuwa mkubwa kuna tisha kama kuzimu, usiogope, waeleze.

     2.   Kuwa makini na mapenzi na yule unayempenda kwanza

Mama, dada, kaka, baba na ndugu zako wengine, wanachukua nafasi ya pili. Nafasi ya kwanza ni wewe mwenyewe.

     3.   Jifunze kuwa mbunifu, siyo mshindani

Ushindani unatumia nguvu nyingi na pesa kuliko ubunifu. Thamani ipo katika ubunifu na siyo ushindani.

     4.   Kuwa na marafiki bila kujali rangi, kabila wala dini

Elewa kwamba, wanaowabagua wengine ni wajinga na kamwe hawapaswi kuigwa.

     5.   Usiamini kila unachosikia

Chunguza ubaini mwenyewe. Usikubali kila kitu, vingine ni uongo uliotungwa na waongo wa dunia.

     6.   Usiende shule ili uajiliwe kazi nzuri, nenda shule ili uwe tajiri

Mfumo wa sasa, utakufanya uajiliwe na bosi ambaye alishindwa mtihani ambao wewe umefaulu. Elimu binafsi itakufanya tajiri.

     7.   Tafuta maarifa

Maarifa ni kitu cha lazima, kuna faida gani ya kuwa na mali, kisha ukaipoteza mali hiyo kwa sababu ya kukosa maarifa?

     8.   Waheshimu wazazi wako

Jinsi unavyowafanyia wazazi wako, watoto wako watakufanyia hivyo hivyo. Ukiwafanyia ubaya, na wao watakufanyia ubaya. Ukiwa mwema, nao watakuwa wema kwako.

     9.   Furahia maisha na usiruke hatua

Hatua ya maisha utakayoiruka, utaifidia uzeeni. Itashangaza ukililia kubebwa mgongoni uzeeni.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie