Maswali ya Semina ya Semantiki na Pragmatiki ya Kiswahili

1. Fafanua aina saba za maana kama zinavyopendekezwa na Leech (1981). Toa mifano ya kutosha na inayoeleweka kwa kila aina ya maneno.

- Maana ya msingi.
- Maana dokezi.
- Maana mwangwi.
- Maana dhamira.

2. Jadili dhana za utajo,urejeleo na dhana kama zinavyotumika katika taaluma ya semantiki.

- Dhana ya utajo.
- Ni ya mwanzo zaidi.
- Umbo la kiisimu hurejelea kitu fulani. Mfano, Juma - kipashio cha kiisimu.
- Maana ni kile kilichotajwa.
- Uhusiano wa jina na kitajwa.
Ubora
- Maneno yanatumiwa kama ni dhana. Mfano, daftari, kalamu n.k
- Inabainisha kuonesha uhusiano uliopo baina ya neno linaloashiria. Embe, chungwa.
- Inaonesha uhusiano mkubwa kati ya kitu kinachotajwa kwa kutumia milio. Mfano, nyau, mtutu.
Mapungufu
- Inatilia mkazo aina moja ya maneno yaani nomino na kushindwa kujitosheleza.
- Si kila neno katika lugha lina kirejeleo katika ulimwengu halisi.
- Kitajwa kimoja kinaweza kuashiriwa kwa maneno tofauti tofauti. Mfano, John Pombe Magufuli. Rais wa Tanzania. Amiri jeshi mkuu.
- Kitajwa kimoja kinaweza kuwa na maana nyingi.
Urejeleo
Ogdan na Richard 1923
- Maana hujitokeza pale kilipo kirejelwa chake.
Ugumu katika dhana
- Si kila kiambo/kileksika na kirejelezi chake, mfano, nomino dhahania kama Mungu, mawazo n.k
- Kunasababisha utata katika kufasili maana ya maana. Mfano, kaa, paa.
- Haifanyi kazi kwenye maneno ya kipolisemia. Mfano, kichwa kimepasuka.
Dhana, maana kama dhana
Ogdan/Richard
- Ni jumla ya mawazo yaliyotokana na mzungumzaji wa lugha katika………….
- Maana ya kitu inaanzia akilini mwa mtu. Mfano, kiti - kifaa cha kukalia
Ubora wa dhana
- Husaidia kutupa maana hata zile maana dhahania.
- Maana za maneno huhusishwana hoja ya ziada.
Upungufu
Haitoshi kuweka msisitizo katika dhana.
Hitimisho
Dhana ya maana ni changamano.

3. Tofautisha uhusiano wa kimlalo na uhusiano wa kiwima. Toa hoja ukiegemeza katika semantiki ya kileksika.

Maana ya leksimu
Tofauti ya mahusiano kiwima na kimlalo
Maana
Kiwima kubadilishana nafasi. Mfano, nomino kwa nomino.
Mfano:
Mtoto analima shamba
Uhusiano kimlalo
Editha anapenda wanafunzi wake.
Kiwima huangalia zaidi maneno pwekepweke katika tungo,mfano, mama anapika chakula. Dada anapika chakula.
Kimlalo hutegemea mahusiano ya kisarufi.
Tofauti katika muundo kategoria katika tungo zinaweza kubadilishana nafasi. Mfano, mtoto mtoro ameadhibiwa. Kijana mzuri amepigwa.
Mahusiano ya kimlalo si lazima yawe na tungo nyingi kutokea hata tungo moja inatosha.
Mahusiano ya kimlalo yanaongozwa na sheria na kanuni. Mfano, dada wazuri.
Mahusiano ya kiwima yanazingatia ukweli, uhakika na uwazi juu ya kinachosemwa.
Hitimisho
Ufanano wa mahusiano ya kiwima na kimlalo
Umuhimu wa kiyambo chochote cha kiisimu ni pale kinapohusishwa na kiyambo kingine.

4. Mahusiano ya kifahiwa maana yake nini? Fafanua jibu lako huku ukitumia aina kadhaa za uhusiano wa kifahiwa, hiponimia, menonimia, sinonimia, antonimia na polisemia.

Hiponimia
Neno moja linakuwa na sehemu ndogo nyingine. Mfano, chuo kikuu cha Dar es Salaam. Ndani yake kuna: TATAKI, COHU, COSS n.k
Menonimia
Unadhihirisha sehemu ya kisemantiki ndani ya kitu kizima. Mfano, betri za simu zina mahusiano.
Homonimia
Muundo wa neno kubeba maana mbili au zaidi.
Habwe na Karanja
Maneno yanafanana katika maumbo lakini hayafanani maana zaidi, mfano, paa, kaa.
Hayana usuli mmoja wa kihistoria.
Polisemia
Neno moja kuwa na maana mbili au zaidi katika lugha. Mfano, mlango, sehemu watu wanapita.
Antonimia
Maneno ambayo maana zakeni unyume.
Mfano, tajiri-masikini
Aina za unyume
Vinyume vya ukanushi
Leksimu hizi huwa na uhusiano wa kiutoano. Mfano: Joto-baridi.
Vinyume vya ukadilifu
Ni vya ukadiliaji
Nene-nyembamba
Ndogo-kubwa
Vinyume vya uelekeano
Huwa ni uhusiano unaoelekeana
Huangalia hali ya tendo linapoelekea
Mfano, nunua
Sinonimia
Inatokana na lahaja mbalimbali ila inaleta maana hiyohiyo.
Daladala
Matatu
Kifodi
Kukopa maneno kutoka lugha nyingine. Mfano: televisheni, kompyuta.
Aina za sinonimia
Kimantiki
Leksimu mbili au zaidi huwa na usawe iwapo zinaweza kubadilisha nafasi.
Sinonimia kamilifu
Leksimu zinaweza kukamilisha usawe kamili.
Visawe vinaweza kutambuliwa kwa kutumia: muktadha, matini…
Uhusiano wa maneno haya husaidia kutoa maneno katika lugha.

5. Onesha jinsi dhana za ukinzani, upotoo pamoja na uziada dufu zinavyokinzana.

Ukinzani ni hali ambayo hujitokeza pale ambapo kitu humaanisha kitu kisicho na sifa hizo.
Mfano, Mzee yule ni motto kabisa.
Upotoo ni ukiushi wa kimantiki.
Mfano, alichora barua kwa kutumia mguu wa kulia.
Upotoo unatokana na neno potoa.
Upotoo unaweza kuwa sahihi kisarufi lakini ukawa na makosa kimantiki. Mfano, wanaume tisa wamebeba mimba.
Dhana hizi zinafanana katika mambo haya:
Zote zipo katika semantiki.
Zinalenga kutoa maana.
Huibua utata miongoni mwa wasikilizaji.

6. Eleza kwa kina na kwa kutoa mifano kuntu maana ya uolezi na aina zake.

Dhana ya uolezi iliazimwa kutoka lugha ya kigiriki.
Kuna aina mbalimbali ya uolezi kama: uolezi wa nafsi, mahali na wakati, uolezi wa jamii na uolezi wa matini.

7. Unaelewa nini kuhusu nadharia ya tendo uneni? Jadili kwa kina masharti ya nadharia hii.

Tendo uneni linatokana na tamko.
Hatua za tendo uneni ni: utamkaji, athari ya tamko, n.k
Aina za tendo uneni ni: kitendo cha madai, kitendo uneni cha masharti, kitendo uneni cha uelezi, kitendo uneni cha maagizo.
Umuhimu wa tendo uneni ni:
Hudhihirisha maana ya tamko katika muktadha mahsusi.
Inasaidia kuelewa maana ya maneno.
Masharti ya nadharia ya tendo uneni:
Kuwepo kwa mazingira maalum
Mpokeaji au msikilizaji sharti lazima awe na muafaka.
Hadhi na mamlaka ya msemaji.
Kuwepo kwa mavazi yanayoendana na uneni husika.
Sharia na taratibu tofauti.

8. Kwa kutumia mifano muafaka ya kutosha, jadili dhima za udhanilizo, umanilizi na uchopezi kama zinavyotumika katika taaluma ya pragmatiki.

Udhanilizo
Msemaji kudhani msikilizaji ana taarifa za awali juu ya taarifa inayosemwa. Mfano: Maji marefu amefaulu.
Haubadiliki hata pale sentensi msingi inapokanushwa.
Haubadiliki hata pale sentensi msingi inapobadilishwa na kuwa sentensi ulizi. Mfano: Mapalala amenunua gari?
Aina za udhanilizo
Udhanilizo wa ukweli
Matumizi ya maneno ambayo hubainisha ukweli. Mfano, sikujua kama Mapunda amefukuzwa kazi.
Udhanilizo wa kileksika
Mfano, Juma amefilisika.
Udhanilizo wa kimuundo
Mfano, wasanii wa pwani wametekwa?
Udhanilizo kinzani
Hudhaniliza uongo na ukweli wa taarifa.
Udhanilizo uso kweli.
Mwalimu ameota amepandishwa cheo.
Uchopezi
Uhusiano wa sentensi mbili, ukweli wa sentensi ya pili ndio ukweli wa sentensi ya kwanza.
Aina za uchopezi
Uchopezi wa kileksika
Uchopezi wa kimuundo
Umanilizi
Umanilizi ni kile kinachomaanishwa katika usemi. Kusema kile usichokitaja.
Aina ya vimanilizi
Mazungumzo
Kaida.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie