Mambo ya Thamani Ambayo Kila Mtu Anatakiwa Kuyafahamu

Alama ya kuuliza.
Kuna mambo ya thamani ambayo kila mtu anapaswa kuyafahamu, kwa hivyo basi, ni hasara kubwa kutokuyafahamu. Mambo hayo ni:

1. Unapocheka, utacheka na watu wengi, lakini pale unapolia, utalia peke yako

Wakati wa furaha, wengi watakuwa na wewe, lakini wakati wa matatizo, hakuna atakayethubutu kusimama na wewe, utabaki peke yako.

2. Matendo yako ndiyo yanayoamua aina ya maisha yako

Kama wewe ni mvivu, kuna uwezekano mkubwa huko mbeleni ukawa masikini wa kutupwa. Tafadhali badilisha matendo yako na anza kuwa na matendo yenye faida katika maisha yako ya baadae.

3. Watendee wengine kama unavyotaka wewe kutendewa

Tenda wema, wema una sifa ya kukurudia. Kutenda ubaya kwa wengine ilhali wewe hupendi kutendewa ubaya, ni makosa. Wapende watu kama unavyojipenda mwenyewe.

4. Siyo kila mtu atakupenda, lakini wapo watakaokupenda

Huwezi kupendwa na watu wote duniani. Lakini habari njema ni kwamba, huwezi kuchukiwa na watu wote.

5. Penda kwa moyo wako wote, na usitegemee kupata chochote

Ukipenda kwa lengo la kupata kitu fulani, kuna asilimia nyingi kuwa, utaishia kuumia. Hivyo ni busara pale unapopenda, penda tu, penda bila sababu, penda bila kutaka kitu fulani, hii itakusaidia mambo yatakapokuendea vibaya katika upendo huo, usipatwe wala kusababisha madhara.

6. Uliza maswali mengi uwezavyo, lakini usiulize swali moja mara mbili

Kuuliza swali lilelile mara mbili ni usumbufu na ni nadra kupata majibu mapya. Kuwa mdadisi uliza maswali mengi upate majibu mengi na ujifunze mengi.

7. Wakati mwingine mambo huwa hayaendi kama ulivyopanga

Siyo kila unalopanga wewe lazima lifanikiwe. Mengine hushindikana, hivyo, jiandae kwa hilo. Maisha siyo furaha tu, na nyakati za hudhuni zipo hivyo jiandae.
Sasa umefahamu mambo ya thamani sana ambayo kila mtu anapaswa kuyafahamu. Ni matumaini yangu kuwa, utabadilika na kuwa kiumbe bora zaidi.
Pia, unayonafasi ya kuwasambazia mambo haya wale unaowajali na ungetamani wawe watu bora zaidi. Ni jukumu letu wote kuhakikisha kuwa, dunia inabaki kuwa sehemu ya kupendeza na isiyokatisha tamaa.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne