Mtihani wa Kiswahili Kidato cha Tatu 2020 1

Nyota angani.

Maelekezo ya Kufanya Mtihani Ili Usahihishwe na Mwalimu:

1. Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
2. Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
3. Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21.
4. Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
5. Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili).

Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 25 05 66 (Daud Mhuli).

Muda saa 2

Jibu maswali yote

Sehemu A (Alama 15)

     1.   Chagua herufi ya jibu sahihi kutoka katika kipengele I hadi V, kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu cha kujibia.

i.             Ni ipi maana ya ngeli?
     A.  Ni upangiliaji wa nomino katika makundi yanayofanana B. Ni mfumo ambao majina yote hupewa kipaumbele na hadhi ya kuwa vitenzi C. ni ubadilishaji wa nomino kuwa vivumishi D. Ni neno lenye asili ya kihaya likiwa na maana ya kunyumbulisha.

ii.            Sentensi ipi kati ya hizi haijazingatia upatanishi wa kisarufi?
A.  Mtoto anacheza uwanjani B. baba wanalima shamba C. rais ana hutubia mkutano D. watoto amelala chumbani

iii.           Huu ni mfano wa kirai nomino
A.  Mtoto yule B. yule mzee C. kwa baba D. Piga mjomba

iv.          Huu ni mfano wa kishazi tegemezi.
A.  Samaki mkunje angali mbichi B. mtoto ameokolewa C. shamba limenunuliwa D. mbuzi aliyekuwa mgonjwa

v.           Huu ni mfano wa sentensi ambatano
A.  Mama anapika chakula B. mtoto aliyelala ameamka C. mama anapika na baba anafua D. Hamis angelijua angenilipa pesa zangu.

Sehemu B (alama 40)
      2.   Eleza kwa ufupi kuhusu madai haya:
i.             Kiswahili ni kiarabu
ii.            Kiswahili ni pijini au kreoli
iii.           Kiswahili ni kikongo
iv.          Kiswahili ni kibantu

     3.   Toa mifano minne ya ushahidi wa kimsamiati unaothibitisha kuwa Kiswahili ni Kibantu.

     4.   Toa mifano minne ya ushahidi wa kimuundo inayothibitisha kuwa Kiswahili ni kibantu.

Sehemu C (alama 45)

     5.   Kwa kutumia mifano, bila kujali mpangilio wake, fafanua aina sita za ngeli kwa kuzingatia kigezo cha upatanisho wa kisarufi.

     6.   Eleza aina tano za virai.

   7.   Jadili aina tatu za sentensi huku ukitoa mifano mitatu kwa kila aina ya sentensi.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie