Mtihani wa Kiswahili 2 Kidato cha Sita 2020 2 Fomati Mpya
Maelekezo ya Kufanya Mtihani Ili Usahihishwe na Mwalimu:
1.
Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
2.
Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
3.
Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya
Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21.
4.
Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
5.
Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili).
Namba
za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 25 05 66
(Daud Mhuli).
Muda:
Saa Tatu
Sehemu A (Alama 40)
Jibu
maswali yote
1.
Orodhesha dhima nne za tamthiliya ya
Kiswahili tangu kupata uhuru mpaka hivi sasa.
2.
Jadili kwa ufupi dhima nne za mhakiki wa kazi
za fasihi.
3.
Kwa kutumia mifano, jadili kwa ufupi jinsi
uandishi wa riwaya ulivyoisaidia jamii yetu. Toa hoja tano.
4.
Soma kwa makini habari hii kisha jadili
vipengele vya fani vilivyotumika:
“Mako, nirejeshe nyumbani, njia iko wapi?” aliuliza
Chimota bila ya salamu. Sikuijua njia ya kurejea nyumbani, nikamtazama
nikitabasamu kisha nikamjibu,
“Siijui njia, nilijikuta niko huku kwa ulozi wa babu
yako, sifahamu kabisa nilifikaje maeneo haya.” Jibu hili lilikuwa baya kabisa
kwa Chimota, alikosa matumaini akakaa chini kwa huzuni. Bila shaka aliyachoka
maisha ya mapambano, alichoka kukaa msituni akiwindwa, alitamani kuwa sehemu
salama nyumbani kwa babu yake.
Tukiwa tumekaa pale tukitafakari namna ya kurejea
nyumbani, tulisikia muungurumo wa kitu kama ndege. Vumbi jingi likatimka.
Chimota aliitazama kwa tahadhari, akataka kushambulia, lakini nikamkamata mkono
wake kumsihi asubiri kwanza tuone ni nani alikuwa akielea katika chombo hicho.
Chombo kilizidi kushuka chini mpaka kikawa sawa na urefu
wangu nikisimama wima, ndani ya Chombo hicho mzee mwenye nywele nyeupe
akachungulia, alikuwa Samike. Mimi na Chimota tukatazamana kwa furaha, Chimota
alimkumbuka babu yake, hakumsahau!
Amri ilitoka ikitutaka tuingie chomboni, nami nikamshika
Chimota, nikamuingiza humo, kisha nikafuata mwenyewe. Sasa tukawa watu watatu
ndani ya chombo kilichopaa. Tulitazamana kwa nyuso za furaha isiyo kifani. Naye
mzee akatamka, “sasa tunarejea nyumbani.” kisha akakichochea chombo tayari kwa
safari.
Lakini kabla chombo hakijachochewa sawasawa, Chimota
akamshika mkono babu yake, akanena kwa sauti tulivu, “hatuwezi kurejea
nyumbani, mama yupo huku, lazima tumuokoe!”
“Mama yako alikufa, kafikaje huku?” Samike aliuliza.
Kabla Chimota hajatoa maelezo, tulimuona msichana akikimbia kuomba msaada,
nyuma, alifukuzwa na askari waliopanda fisi. Samike alimtambua msichana yule,
alikuwa mtoto wake wa pekee. Chimota alimtambua msichana yule, alikuwa mama
yake mzazi. Nami nilimtambua msichana yule, alikuwa mpenzi mpya niliyempata
matekani!
Chimota hakutaka mchezo mbele ya binti yake, akarusha
kombola kali, askari na fisi wakaanguka chini. Kama ilivyokawaida yao, wachache
waliobaki, wakarudi nyumbani!
Tulimchukua binti yule, alipokaa, tukatazamana kwa aibu!
Samike akaondoa chombo kwa kasi, mengi aliyokuwa nayo, angeyasema tukifika,
hakutaka kuzungumza, alijali usalama wetu. Nami nikawaza, “sasa nimepata mke,
mimi si popo tena, mimi ni shujaa Mako!”
Sehemu B (Alama 60)
Jibu maswali matatu. Swali moja lazima
litoke katika ushairi.
5.
“Waandishi wana kazi moja tu, kupiga vita
mambo yanayozuia maendeleo ya jamii.” Jadili ukweli wa kauli hii kwa kutumia
diwani mbili ulizosoma. Hoja tatu kwa kila diwani.
6.
Jadili miundo mitatu tofauti ya mashairi kwa
kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma.
7.
Jadili dhamira zenye uhalisia katika riwaya
mbili ulizosoma. Tumia hoja tatu kwa kila kitabu.
8.
Chagua wahusika wawili kutoka kila
tamthiliya, kisha eleza wasifu wao. Toa hoja tatu kwa kila kitabu.