Mtihani wa Kiswahili 1 Kidato cha Sita 2020 2 Fomati Mpya

Maelekezo ya Kufanya Mtihani Ili Usahihishwe na Mwalimu:

1. Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
2. Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
3. Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21.
4. Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
5. Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili).
Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 25 05 66 (Daud Mhuli).
Muda: Saa Tatu

Sehemu A (Alama 40)

       1.   Soma kwa makini kifungu hiki cha habari kisha jibu maswali yanayofuata:
Bwana Mako alinyanyuka katika sofa, akarusha mateke na ngumi mfululizo mpaka alipohisi yupo sawa kwa mapambano. Mwenye uchungu na nchi yake, alikisogeza pembeni kitanda, kisha akafunua chini katika sakafu, humo alificha siraha zake nyingi za maangamizi. Aliamua kuchukua siraha mojawapo, bunduki ya kisasa, Norinco 97, akaifuta vumbi na kuirudisha pahala pake. Alipomaliza ukaguzi wa siraha, akapanga kila kitu kama kilivyokuwa awali, kisha akachukua simu yake na kumwandikia ujumbe mfupi Lightness, “kazi imeanza.”

Nchi ya Andalasu ilikuwa katika shida kubwa. Mgodi pekee uliotegemewa na taifa hili masikini, ulivamiwa na kundi la wanyang’anyi waliokuwa na siraha za moto. Haikufahamika ni nani alikuwa nyuma ya kundi hili. Kwa kuwa mgodi huu unaotoa Almasi kwa wingi kuliko mgodi wowote ule Duniani ulikuwa mikononi mwa wanyang’anyi, serikali ilipoteza fedha nyingi na ilianza kushindwa kujiendesha, hali ilikuwa mbaya katika serikali na uchumi wa nchi nzima.

Mgodi ulipotekwa mara ya kwanza, kilitumwa kikosi cha askari kwenda kuukomboa, askari wote waliuawa. Baada ya hapo kikatumwa kikosi cha makomando, ambacho nacho kilifyekelewa mbali na hakuna aliyebaki. Vikosi vingi viliendelea kutumwa na matokeo yalikuwa yaleyale, hakuna aliyerudi akiwa hai. Serikali ikawa katika hofu kubwa ya wanyang’anyi hawa wasiofahamika.

Vikosi vingine vilipotumwa kwenda kupambana na wanyang’anyi hawa, vilikataa kwa kutoa sababu kuwa, silaha walizotumia wao zilikuwa za kiwango cha chini mno ukilinganisha na wanyang’anyi ambao wao walitumia silaha kali zaidi. Wakati askari wa serikali wakienda kuvamia wakiwa na siraha aina ya SMG yenye uwezo wa kubeba risasi 30, wanyang’anyi walitumia siraha za maangamizi kama IWI X95 TAVOR ambayo iliweza kupiga risasi 950 kwa dakika! Mwenye nguvu mpishe!

Maswali

     a.   Andika kichwa cha habari hii kwa maneno yasiyozidi matatu.

     b.   Toa maana ya maneno haya kama yalivyotumika:
i.             Sofa
ii.            Siraha
iii.           Mgodi
iv.          Wanyang’anyi
v.           Askari

    c.   Usemi, ‘mwenye nguvu mpishe, una maana gani?’

    d.   Taja funzo moja ulilolipata katika habari hiyo.

    2.   Eleza faida tano za kujifunza sarufi ya Kiswahili.

    3.   kwa kutumia mifano, eleza maana ya istilahi zifuatazo:
i.             mofimu
ii.            mofimu huru
iii.           viambishi
iv.          mzizi

    4.   huku ukitoa mifano, taja mitindo mitano ya lugha kutokana na mazingira.

Sehemu B (Alama 60)


Jibu maswali matatu, swali la 8 ni la lazima

    5.   Andika insha ya hoja kuhusu mada isemayo, ‘Faida za mazoezi.’

    6.   Kwa kutumia hoja sita, tathmini hoja zinazodai kwamba kiswahili ni kiarabu, pijini au kreoli.

    7.   Fafanua maana na matumizi ya lugha ya kwanza, pili, rasmi na lugha ya taifa.

    8.   Tafsiri matini hii ya Kiingereza, kuwa katika lugha ya Kiswahili:

I’m told that there once was a stranger from some other town who was walking in a plantation along the coast. As he walked along, he suddenly saw a very pretty little necklace lying on the road. He snatched up the necklace and threw it into his mouth because there was another person walking behind him and he didn’t want him to see the necklace. The necklace was really a snake. He died immediately. He died because he didn’t realize that it was a snake; he didn’t know he put a snake into his mouth rather than a necklace.Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie