Kiswahili Online Examination Kidato cha Nne 2 2019

darasa tupu

Endapo unataka kufanya mtihani huu ili usahihishwe na Mwalimu, zingatia mambo haya:

1. Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
2. Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
3. Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21.
4. Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
5. Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili).
Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 25 05 66 (Daud Makoba)
“Kwa kuwa lengo la mtihani huu ni kutaka kujua uwezo na mapungufu ya mwanafunzi ili aweze kupewa mbinu mbadala za kumsaidia kufaulu mtihani wake wa mwisho, kufanya udanganyifu hakuna faida yoyote kwani lengo la mtihani si kubaini nani atakuwa wa kwanza na yupi atakuwa wa mwisho!”
It is far more honorable to fail than to cheat.
Sasa fanya mtihani wako…

Muda: Saa 2.30
Maelekezo:
1. Jibu maswali yote isipokuwa kama imeelekezwa vingine katika maelekezo ya kipengele cha swali husika.
2. Andika jina lako katika kila ukurasa wa karatasi yako ya kujibia.
3. Kwa manufaa yako, usifanye udanganyifu.

Sehemu A (alama 10)  (Ufahamu)

1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Ugonjwa wa homa ya Dengue ni ugonjwa ambao unasambaa kwa kasi nchini Tanzania. Watu wengi wameambukizwa na wengine wamepoteza maisha kwa sababu ya ugonjwa huu.
Ugonjwa wa homa ya dengue unasababishwa na mbu na kinga pekee ya kuzuia homa hii, ni kuepuka kung’atwa na mbu aenezae homa ya dengue. Sasa watu wapo katika taharuki wakihofia ugonjwa huu.
Dalili za homa ya dengue ni pamoja na: homa kali ya ghafla, maumivu ya kichwa, macho kuuma, maumivu ya shingo, kichefuchefu, kutapika, kutokwa na vipele na kutokwa na damu puani. Ukiona dalili hizi kimbia haraka hospitali kufanya vipimo.
Ugonjwa huu kwa kiasi kikubwa unarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu, hivyo, hatua za makusudi zinatakiwa zichukuliwe kupambana na janga hili.
Wananchi wanashauriwa kuangamiza mazalia ya mbu, hii ni njia pekee ambayo itazuia kusambaa kwa ugonjwa huu.
Hakuna dawa maalumu ya kutibu homa ya dengue, hata hivyo, matapeli wameshaanza kujitokeza wakidai wanadawa iliyotengenezwa kwa majani ya mpapai, yote hii ni kutaka kuwaibia wananchi.
Hata hivyo, wagonjwa wanashauriwa kunywa maji mengi na panadol kwani kwa kufanya hivyo, wanaweza kupata nafuu na kupona.
Ni wito wangu kwa serikali kuingilia kati tatizo hili kwa kuwasaidia wananchi kupuliza dawa itakayoangamiza mbu. Kwa kufanya hivyo, dengue itabaki historia!

Maswali

A. Eleza sababu moja inayosababisha homa ya dengue
B. Taja dalili tatu za homa ya dengue
C. Taja sababu moja itakayoondoa kabisa homa ya dengue
D. Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma
2. Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua 100 na kuzidi 120.

Sehemu B (Alama 25)  Sarufi na Utumizi wa Lugha

3. Bainisha aina za maneno zilizopo katika sentensi zifuatazo:
I. Amina anacheza mpira uwanjani.
II. Baba na mama wanakwenda sokoni.
III. Yule mzuri kaacha shule.
IV. Watoto wetu wamelala usingizi.
V. Samaki huyu amekunjwa akiwa mbichi.
4. Taja majina mengine mawili ya neno ‘fedha’.
5. Taja maana ya maneno haya
I. Kikongwe
II. Gubu
III. Seremala
IV. Jeneza
V. Kaburi

Sehemu C (Alama 10)  Uandishi

6. Eleza tofauti tano zilizopo kati ya insha za kisanaa na zile zisizo za kisanaa.

Sehemu D (Alama 10)  Maendeleo ya Kiswahili

7. Eleza ukuaji wa Kiswahili kimsamiati katika enzi ya Waarabu.

Sehemu E (Alama 45)  Fasihi kwa Ujumla 

(Jibu maswali matatu, swali la 12 ni la lazima)

8. Ukitumia maelezo mengi na mifano, fafanua aina mbili za fasihi.
9. “Washairi waandikapo kazi zao, huyatazama yale yaliyopo katika jamii na kuyaweka katika mashairi.” Fafanua ukweli wa kauli hii ukitumia diwani mbili ulizosoma. (Hoja tatu kwa kila kitabu.)
10. “Kila riwaya lazima iwe na dhamira fulani zilizomsukuma mwandishi kuandika kazi yake.” Jadili ukweli wa kauli hii ukitumia riwaya mbili ulizosoma.
11. “Tamthiliya ni mwigo wa mambo yatendekayo katika jamii.” Kubali kauli hii kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma. (Hoja tatu kwa kila kitabu).
12. Kwa kutumia mifano, pambanua mikondo mitano ya hadithi.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne