Uhakiki wa Tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
JINA LA KITABU: NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE MWANDISHI: EDWIN SEMZABA Mhakiki: Mwalimu Makoba Utangulizi Afisa aliyetumwa kuhesabu watu-Ngoswe, anashindwa kuifanya kazi yake na kuanzisha ajenda nyingine ya mapenzi. Anapanga kutoroka na binti Mazoea aliyekwisha kuposwa tayari, Mazoea naye kusikia atakwenda kuishi mjini anakubaliana na mpango huo. Wanapotoroka, Ngoswe anasahau mkoba wenye takwimu za watu waliokwisha kuhesabiwa, Mzee Ngengemkeni Mitomingi ambaye ndiye baba yake na Mazoea, anazichoma moto takwimu hizo na kumsababishia hasara kubwa Ngoswe. J ina la Kitabu Jina la kitabu “Ngoswe penzi kitovu cha uzembe” ni jina ambalo limesawiri vyema yaliyomo ndani ya kitabu hicho, kwani Ngoswe ndio jina la mhusika mkuu anayebeba dhamira kuu ya tamthiliya. Pia penzi limeonekana kuwa ni kitovu cha uzembe kwani ndio yaliyopelekea kuteketezwa kwa karatasi za takwimu za sensa. Hivyo jina la kitabu si tu kwamba limesawiri yaliyomo katika kitabu bali pia katika jamii. Maudhui ...