Huwezi kufaulu mtihani bila kuangalia mitihani ya NECTA au inayofanana nayo na jinsi inavyojibiwa. Chini, nimekuwekea Review kulingana na masomo mbalimbali, chagua mitihani unayotaka kisha soma.
MWANDISHI: EMMANUEL MBOGO WACHAPISHAJI: HEKO PUBLISHERS MWAKA: 2002 MHAKIKI: MWALIMU MAKOBA Wasifu wa Mwandishi Emmanuel Mbogo ni Profesa wa drama na fasihi na amehudumu katika vyuo vikuu mbalimbali ikiwemo, Chuo Kikuu cha Kenyatta Kenya na Chuo Kikuu Huria. Mbogo ni mwanafasihi mahiri sana katika Afrika ya Mashariki. Muhtasari wa Riwaya Maman’tilie, mama mwenye watoto wawili lakini wote wamefukuzwa shule kwa kukosa ada na sare. Anajitahidi hapa na pale ili apate, lakini wapi? Pesa imegeuka nyoka inateleza kwenye nyasi. Mumewe Mzee Lomolomo hana muda, yeye kila kukuchapo huelekea bunge la walevi kunywa pombe tani yake. Akiwa huko hunywa na kurudi nyumbani akiwa mbwii! Mwisho mwandishi anauliza swali gumu, ‘Nani anajali?’ Uchambuzi wa Fani na Maudhui Maudhui Katika Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie Maudhui hujumuisha mawazo na pengine mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma mtunzi ama mwandishi wa kazi ya fasihi akaandika kazi yake. Dhamira Dhamira ni lile wazo linalom...
TAMTHILIYA; KILIO CHETU MWANDISHI; MEDICAL AID FOUNDATION MCHAPISHAJI; TANZANIA PUBLISHING HOUSE MWAKA; 1995 JINA LA MHAKIKI; Mwalimu Daud Makoba Kilio chetu ni tamthiliya inayovunja ukimya uliotawala miongoni mwa jamii katika kutatua matatizo makubwa ambayo chimbuko lake ni mahusiano ya kijinsia. Katika tamthiliya hii vijana wanatoa sauti ya jitimai iliyojaa sononeko na shutuma dhidi ya wazazi, walezi na viongozi ambao wanafumbia macho suala hili nyeti. Ndiyo maana tamthiliya hii inasisitiza sana haja ya kuwapa vijana elimu juu ya mahusiano ya kijinsia badala ya hofu na vitisho ambavyo vimedhihirika kupitia hali halisi ya kuwa vimeshindwa. FANI MUUNDO Tamthiliya hii imetumia muundo wa moja kwa moja. Inaanza kwa kutuonesha wazazi wakibishana juu ya kutoa elimu ya jinsia na mahusiano. Mwisho Joti mtoto ambaye hakupatiwa elimu hiyo anampa mimba mtoto mwenzake Suzi. Baadae Joti anakufa kwa UKIMWI. Pia tamthiliya hii imegawanywa katika sehemu sita. sehemu y...
JINA LA KITABU: NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE MWANDISHI: EDWIN SEMZABA Mhakiki: Mwalimu Makoba Utangulizi Afisa aliyetumwa kuhesabu watu-Ngoswe, anashindwa kuifanya kazi yake na kuanzisha ajenda nyingine ya mapenzi. Anapanga kutoroka na binti Mazoea aliyekwisha kuposwa tayari, Mazoea naye kusikia atakwenda kuishi mjini anakubaliana na mpango huo. Wanapotoroka, Ngoswe anasahau mkoba wenye takwimu za watu waliokwisha kuhesabiwa, Mzee Ngengemkeni Mitomingi ambaye ndiye baba yake na Mazoea, anazichoma moto takwimu hizo na kumsababishia hasara kubwa Ngoswe. J ina la Kitabu Jina la kitabu “Ngoswe penzi kitovu cha uzembe” ni jina ambalo limesawiri vyema yaliyomo ndani ya kitabu hicho, kwani Ngoswe ndio jina la mhusika mkuu anayebeba dhamira kuu ya tamthiliya. Pia penzi limeonekana kuwa ni kitovu cha uzembe kwani ndio yaliyopelekea kuteketezwa kwa karatasi za takwimu za sensa. Hivyo jina la kitabu si tu kwamba limesawiri yaliyomo katika kitabu bali pia katika jamii. Maudhui ...