Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi. CV au wasifu ni kitu cha lazima kwa yeyote anayeomba kazi. Watu wengi wanaokosa kazi, tatizo huwa siyo wao, bali tatizo huwa ni CV zao. Kumekuwa na makosa mengi katika uandishi wa CV jambo ambalo limesababisha watafuta kazi wengi kushindwa kuitwa kwenye usaili. Makala hii itakueleza namna sahihi ya kuandika CV, utaitwa katika ‘interview’ nyingi endapo utaandika CV sahihi. Tena nakukumbusha, kila taaluma ina aina yake ya CV, CV ya rubani haifanani na CV ya injinia. Vivyo hivyo, CV ya mpishi haifananani na CV ya Mwalimu. Pia nakukumbusha usome jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi , kwani CV huenda pamoja na barua ya maombi ya kazi. CV Bora ni Ipi? Ukurasa Mmoja au Kurasa mbili hadi tatu? CV bora ni ile yenye kurasa mbili hadi tatu. Watu wengi wanapojifunza namna ya kuandika CV, wamekuwa wakiona CV zenye ukurasa