Biology Form One Notes New Syllabus

Two students holding biology form one notes

Hizi Hapa Notes Zote za Biology Form One Silabasi Mpya:

1. Introduction to Biology

2. Scientific Processes in Biology

3. Cell Structure and Organisation

4. Classification of Living Things

5. Viruses and Major Groups of Living Things

6. Nutrition in Plants

Jipatie Kitabu Chenye Notes Zote za Biology Form One Silabasi Mpya, Wasiliana na Mwalimu kwa Kugusa Hapa

Mada ya kwanza inahusu utangulizi wa somo la Biology, katika utangulizi huu utajifunza maana ya biology pamoja na faida za kusoma somo hili.

Mada ya pili inaeleza kuhusu hatua mbalimbali zinazofanyika katika majaribio ya kibaiolojia. Hapa utaweza kuifahamu maabara ya biology inafananaje pamoja na vifaa vinavyotumika humo na sheria nyinginezo.

Mada ya tatu utafahamu kuhusu seli, kitu kidogo kabisa kinachotengeneza kiumbe hai kama mtu.

Mada ya nne utajifunza makundi ya viumbe hai. Viumbe hai huweza kugawanywa katika makundi mbalimbali kulingana na sifa wanazofanana.

Mada ya tano utajifunza kuhusu virusi na makundi mbalimbali ya viumbe hai. Ni katika mada hii tutabaini kwamba, virusi ana sifa zote mbili, sifa za kiumbe hai na sifa za kiumbe kisichokuwa hai.

Mada ya sita utajifunza kuhusu lishe. Lishe hii itahusu mimea. Utajifunza mahitaji muhimu yanayohitajika katika mumea ili uweze kukua.

Katika silabasi mpya, wanafunzi wanajengewa ujuzi mbalimbali utakaowawezesha kuutumia katika mazingira yao kutatua changamoto mbalimbali.

Kwa mfano katika mada ya sita, wanafunzi wanapata ujuzi mkubwa juu ya utunzaji wa mimea. Watafahamu mmea unahitaji nini ili uweze kukua. Kwa mfano, watapata ujuzi kwamba, mmea unahitaji hewa safi ya oksijeni, haidrojeni, mwanga wa jua na mahitaji mengine mengi ili uweze kukua vyema. Watajifunza dalili za mmea ambao una afya nzuri na dalili za mmea ambao una afya iliyozorota. Wakiingia katika kilimo, wanafunzi watatumia ujuzi walioupata kuhudumia vyema mimea yao hivyo kuweza kuongeza mazao.

Mada hizi hazifundishwi kwa kukalili tu, yapo majaribio katika kila sura. Wanafunzi watafanya majaribio mbalimbali makubwa na madogo. Katika lishe ya mimea, watafanya majaribio ya kubaini kama majani yana ‘stachi’ au la. Na katika makundi ya wanyama, watafanya majaribio mbalimbali yatakayowasaidia kuwatofautisha wanyama hao.

Popular posts from this blog

SMS 20 za Vichekesho Zinazochekesha Sana

Vichekesho vya Kuchekesha na Kuvunja Mbavu 1

Uhakiki wa Tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe