Vichekesho vya Kuchekesha na Kuvunja Mbavu 2

Mwanamke anacheka.

1. Chomoa hela kidogo kwenye ada ya mwanao kisha kunywa bia. Elimu haina mwisho.

2. Mtu unamdai halafu anakujibu kwa kiingereza.

3. Kuna mwizi amekamatwa hapa amepewa kipigo. Anaulizwa ataje mwenzake anaanza kuniangalia mimi, nimempiga bonge la kofi.

4. kukosa hela vibaya sana, hata ndoto unazoota zinakuwa hazikuheshimu. Mimi kweli ni wa kuota nakimbizwa na Kinyonga!

5. Nilikuwa siamini kama kila kitu kinawezekana hapa Duniani mpaka siku nilipoota nakimbizwa na konokono.

6. Usikate tamaa kwa sababu kakuambia ana mtu wake. Watu hufariki.

7. Mjomba katoka kijijini, nipo naye katika mgahawa, naagiza chipsi kavu kwa ajili yake na mimi, chipsi zinaletwa. Baada ya kula mara tatu mjomba anavunja ukimya.

“Mjomba,” mjomba ananiita.

“Naam,” naitika nikila chipsi zangu.

“Uliagiza chipsi kavu?”

“Ndiyo.”

“Sasa kwa nini zina mafuta mafuta?

Nilitumia dakika tisini kumuelewesha.

8. Nilialikwa na jamaa kula chakula cha mchana nyumbani kwake. Nilipofika nikakutana na watu wengine waliokuwa nao wamealikwa. Tulipoanza kula, jamaa akachukua simu yake, akapiga ‘video call’ kwa rafiki yake, ‘video call’ ilipopokelewa akasema,

“Unaona kaka, ni kawaida yangu kabisa kula na masikini… unawaona!”

Nilitafakari nisuse chakula au niendelee. Nikaamua niendelee tu kwa sababu kama kudhalilika tayari nimeshadharirika.

9. Niliachwa na mpenzi kwa sababu ya ajabu sana. Alikuja kunitembelea kisha akaniomba nimpeleke sehemu ambayo hajawahi kupelekwa. Basi nikampeleka kumtembeza makaburini. Tuliporudi akasema hawezi kuwa na mahusiano na mchawi, akaniacha.

10. mwaka mmoja nilivamiwa na chatu mkubwa nyumbani kwangu. Nikawapigia simu watu wa maliasili kuwa, waje kumchukua ndani ya dakika arobaini na tano, wasipofanya hivyo wasije. Walichelewa kuja, wakakuta mimi na familia yangu tunakula mishkaki ya chatu.

11. Alikuwa mfupi, nikampenda hadi akarefuka, lakini bado aliniacha mpuuzi yule.

12. Bidii uliyonayo katika kupigania mahusiano yako yasife, ukiiweka kwenye kazi unakuwa bilionea.

13. Walisema mapenzi hayachagui umri, cheo wala kabila, lakini hawakusema hayachagui sheria, hivyo tukikukamata una mahusiano na mwanafunzi tunakufunga.

14. Nguvu unazotumia kupigania mahusiano yako yasife, ukizihamishia kwenye kilimo unalisha Afrika nzima.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu