Notes za History Form One | Kidato cha Kwanza

Namba 1

Notes za History kidato cha kwanza ni:

Sources and importance of history ni mada ambayo inazungumzia vyanzo mbalimbali tunavyoweza kuvitumia ili kupata historia ya mahali fulani. Vyanzo hivyo ni kama: masimulizi ya mdomo, makumbusho na masalia ya viumbe wa kale. Pia, mada hii inaeleza faida za kusoma somo la Historia.

Evolution of man, technology and environment ni mada ambayo inahusu jinsi mwanadamu alivyobadilika kutoka umbo lililofanana na nyani, mpaka alivyo leo hii. Pia, mada hii inagusia suala la mabadiliko ya kiteknolojia kutoka matumizi ya dhana za mawe mpaka kufikia kutumia dhana za chuma na teknolojia nyinginezo.

Development of economic activities and their impact ni mada inayozungumzia maendeleo ya shughuli za kiuchumi kama kilimo na biashara. Mada hii imejadili kwa kina jinsi jamii za kiafrika zilivyokuwa zikiendesha uchumi wake.

Development of social and political system ni mada ambayo inahusu jinsi jamii za kiafrika zilivyokuwa zinajiongoza. Zipo jamii ambazo zilikuwa zinajiongoza katika mifumo ya ukoo, na zipo jamii ambazo zilifikia hatua ya kua na wafalme wake wenyewe. Jamii ambazo zilijitawala kwa kuzingatia umri na jinsia, hazijasahaulika katika mada hii.

Mada hizo nne za history kidato cha kwanza, zinatakiwa zisomwe kwa makini na mwanafunzi ili aweze kupata mambo ambayo yamelengwa. Mbali na kuweza kufaulu mtihani wake, mwanafunzi atapata maarifa yatakayomsaidia katika jamii yake endapo tu, atazielewa kwa kina mada hizo.

Pia, mwanafunzi anashauriwa afanye maswali ya kujipima ambayo yapo mwishoni mwa kila mada. Maswali hayo ndiyo yatampa uhakika kama anaelewa anachokisoma au haelewi.

Notes hizi, zimetumia lugha rahisi ambayo wanafunzi wengi wanaweza kuimudu na kuelewa. Hivyo ni matumaini yangu kuwa, notes hizi zinakwenda kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na walimu.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu