Ni Somo Gani Kubwa Maisha Yamekufundisha?

Ua katika mawe.
Nilikuwa katika kiota cha burudani, humo nilikwenda kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa rafiki yangu mmoja ambaye tumefahamiana kwa miaka dahari. Katika meza niliyokaa, tulikaa wawili, mimi na dada mmoja ambaye hatukuwahi kuonana kabla. Hata hivyo, haikuchukua muda kufahamiana na kuanzisha mazungumzo.

Wakati sherehe ikiendelea, dada aliniuliza swali, “Mwalimu Makoba, ni somo gani kubwa maisha yamekufundisha?”

Nilitafakari kidogo, kisha nikajibu:

“Nimejifunza kwamba hakuna njia ya mkato katika maisha.

Watu wenye miili mizuri isiyo na vitambi wala unene kupitiliza wanastahili. Siyo uchawiWamefanikiwa kwa maamuzi waliyofanya ikiwemo kupangilia mlo na kufanya mazoezi.

Watu wenye mafanikio wanastahili. Mafanikio hayaji kwa bahati tena hayatokei kwa usiku mmoja. Wamefanikiwa kwa sababu waliamua kufanikiwa.”

Nilimaliza kuzungumza, nikabaki kusikiliza mziki na kusukuma mafunda kadhaa ya kinywaji nilichopewa. Nilimsikia dada akirudia maneno niliyosema,
“HAKUNA NJIA YA MKATO KATIKA MAISHA.”


Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne