Mitindo Rahisi Tisa ya Maisha kwa Wanafunzi

Mwanafunzi akiwa peke yake.
Kwa mwanafunzi, siyo rahisi kupata mitindo ya maisha iliyosahihi kwa afya ya mwili na akili. Hapa nimekuwekea mitindo sahihi itakayokufanya uwe na afya bora wakati ukifurahia masomo yako. 

     1.   Usile kupita kiasi

Hata kama hukula chakula cha mchana, haina maana ule kupita kiasi ili kulipa chakula ambacho hukula. Kula kwa kiasi ni jambo jema na kula kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.

     2.   Kula mboga za majani

Kula viazi, mahindi, mboga na vyakula vyenye protini kama samaki na maharage.

     3.   Usinywe pombe

Unywaji wa pombe kupita kiasi hauwezi kukufanya mwenye afya. Pia epuka kula vyakula vyenye sukari kupita kiasi, vyakula hivi ni chanzo cha maradhi na husababisha unenepe.

     4.   Weka malengo

Unapofanya jambo bila kuweka malengo, huwezi kuwa na ari ya kufanya jambo hilo. Weka malengo katika kila jambo unalofanya, kwa mfano kama unafanya mazoezi, weka malengo, malengo ya kufanya mazoezi yanaweza kuwa: kupunguza unene, kuwa na afya, kuondoa hofu au malengo mengine.

     5.   Fanya mazoezi mara kwa mara

Mazoezi yanatufanya wenye afya. Hata mimi hufanya mazoezi, kwa sababu ya kazi nyingi, ratiba yangu ya mazoezi ni rahisi. Unaweza kufuata ratiba yangu? Jumapili huwa nakimbia kiasi cha kilometa 8. Jumatatu sifanyi mazoezi. Jumanne asubuhi pale ninapoamka hupiga pushapu ishirini, huruka kamba mara 200 na hufanya mazoezi ya kukata tumbo. Jumatano na alhamisi sifanyi mazoezi, Ijumaa nafanya mazoezi yale niliyofanya Jumanne. Jumamosi sifanyi mazoezi kisha jumapili nafanya zoezi lile nililokwambia, kukimbia kilomita 8.

     6.   Fanya jambo moja kwa wakati

Ni bora kufanya jambo moja ukalikamilisha kisha ukafanya jambo jingine. Ukifanya mambo mengi kwa wakati mmoja, kuna hatari ya kufanya makosa mengi na kushindwa kuyamaliza mambo hayo. Kama unasoma, tumia muda huo kusoma na siyo kuchat na marafiki.

     7.   Tumia mbinu sahihi kupambana na msongo wa mawazo

Huwezi kuuzuia msongo wa mawazo, hofu na mawazo mabaya. Hata hivyo, unaweza kupambana na vitu hivi hata visiweze kukusumbua. Njia mojawapo ni kujumuika na marafiki, kuzungumza na mtu na tiba nyingine ni kufanya kazi yoyote.

     8.   Usiache kulala

Wanafunzi wengi hudhani kukesha wakisoma ndiyo kupata maarifa. Unakosea sana kama unafanya hivi. Miili yetu huhitaji kupumzika kwa kupata usingizi. Hivyo, hakikisha unalala na kamwe usikeshe ukisoma.

     9.   Kitanda chako kiwe sehemu ya kulala pekee

Usifanye jambo lolote kitandani isipokuwa kulala. Usisome kitandani wala kutumia simu yako, ukifanya hivyo, utafanya kitanda chako kiwe sehemu mpya ya msongo wa mawazo.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu