Jinsi ya Kuongeza Kujiamini

Mtu anayejiamini.
Kushindwa kujiamini ni sababu ya watu wengi kushindwa kupata mafanikio. Inawezekana hukufanya ile biashara ambayo sasa imemtajirisha fulani kwa sababu wewe hukujiamini ulipokuwa na wazo hilo. Unaweza kukosa mengi kwa kushindwa kwako kujiamini. Endapo unataka kuongeza uwezo wa kujiamini, fanya mambo haya:

     1.   Acha uongo

Unashusha heshima yako pale unaposema uongo. Siku zote zungumza ukweli hata kama hauna faida kwako.

     2.   Kuwa makini na ahadi zako

Kama ukisema utafanya jambo fulani, lifanye jambo hilo. Unatakiwa kuwa mtumwa wa maneno yako. Kujiamini kunakuja pale unapoaminika, je unaweza kumuamini mtu anayekudanganya? Bila shaka hapana. Timiza ahadi zako, itaongeza uwezo wa kujiamini.

     3.   Kuwa na watu wanaojiamini

Ukizungukwa na panya, na wewe utakuwa panya. Siku zote zungukwa na watu wanaojiamini, nawe utajiamini.

     4.   Badili fikra zako

Je fikra zako zinakujenga au zinakubomoa? Kama zinakubomoa, badilisha fikra zako. Fikria mambo mazuri na si mabaya.

     5.   Weza kitu fulani

Ukiweza utajiamini. Ongeza uwezo wa kufanya kitu fulani. Inaweza kuwa: kufundisha, kupaka rangi,kutengeneza vitanda na mambo mengine mengi. Yote haya kama huyawezi kwa ufasaha, ni lazima uwe na hofu. Ukiyaweza, utajiamini.

     6.   Fanya mambo yanayokutisha

Safiri. Hutubia. Jifunze kucheza muziki. Fanya mambo yanayokutisha.

Kwa kuzingatia mambo hayo, natumaini uwezo wako wa kujiamini utaongezeka na kukupeleka katika mafanikio ya kweli ambayo kwa muda mrefu umeyakosa kwa sababu ya kukosa kujiamini.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie