Tabia Saba Unazotakiwa Kuwa Nazo Katika Maisha

Uteuzi mzuri wa tabia utakufanya ufanikiwe katika maisha yako. Zifuatazo ni tabia saba ambazo unatakiwa kuwa nazo katika maisha yako, kama huna tabia hizi, tafadhali anza leo kuwa nazo.
1. Usiamini katika kushindwa. Kushindwa siyo mwisho wa kila kitu. Kushindwa kupo siku zote. Ukishindwa, usikate tamaa, endelea kupambana, endelea kufanya kazi. Kitakachotokea ni mafanikio.
2. Lala na amka mapema. Hii ni njia ambayo itasaidia kuongeza udhalishaji mali. Kama jinsi mwili wako unavyohitaji chakula, ndivyo unavyohitaji kupumzika. Kamwe usifanye kazi kupita kiasi hata ukakosa muda wa kulala. Angalau lala saa sita. Kama una muda saa saba, na kama una muda zaidi lala hata saa nane. Amka mapema na fanya kazi. Ukilala muda wa kutosha, utaweza kuwa na ufanisi mkubwa kazini kuliko yule asiyelala muda wa kutosha.
3. Fanya mazoezi. Jali afya yako. Kuna watu wanatamani wangefanya mazoezi mapema kulinda afya zao. Piga pushapu, ruka kamba, kimbia au hata tembea mwendo mrefu. Hii itakufanya uwe mwenye afya ya mwili mpaka akili.
4. Usiwachukie adui zako. Wachukulie kuwa wao ni jambo la kawaida na achana nao. Endapo utawachukia na kuanza kuwafikiria siku nzima, atakayepata hasara ni wewe: kwanza hutafanya kazi kwa ufanisi, na pili utapoteza furaha yako kwa kuruhusu mawazo ya chuki kuhusu adui zako.
5. Kunywa maji ya kutosha. Angalau kunywa lita mbili kwa siku. Kushauriwa kunywa maji ya kutosha haimaanishi unywe maji mengi bila kipimo, maji yakizidi mwilini yanaleta madhara hivyo hakikisha unakuwa na kipimo sahihi. Njia sahihi ya kunywa maji ya kutosha bila kulea madhara ni kuusikiliza mwili wako, pale unapohisi kiu, kunywa maji.
6. Ukipata wazo, liandike, usiliache lipotee. Mawazo ni utajiri. Ukipata wazo juu ya kifu fulani, andika wazo hilo kwani usipofanya hivyo, kuna uwezekano wa wewe kusahau na hatimaye wazo lako kubwa ambalo pengine lingeisaidia Dunia kupotea.
7. Usitumie simu wakati wa chakula. Wakati wa chakula, hutakiwi kuwa na mambo mengi. Kuna mengi yatakupita pale utakapokula huku unatumia simu yako. Kwa wenye familia, muda wa chakula ndiyo mwafaka kwa majadilino kuhusu familia yako. Huu ndiyo wakati wa kuzungumza kuhusu mambo fulani.
Tabia hizo ni mwangaza wa mafanikio. Tabia hizo ni mafanikio yenyewe. Kamwe usikubali kuwa na tabia hatarishi ambazo muda wowote zinaweza kukudhuru. Badala yake kuwa na tabia rafiki, nzuri ambazo zitaweza kukufaidisha muda wowote.

Popular posts from this blog

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne