Mtihani wa Kiswahili 2 Kidato cha Sita 2020 1 Fomati Mpya

Cheche za fataki.

Maelekezo ya Kufanya Mtihani Ili Usahihishwe na Mwalimu:

1. Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
2. Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
3. Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21.
4. Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
5. Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili).
Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 25 05 66 (Daud Mhuli).

Muda: Saa 3

Sehemu A (alama 40)

Jibu maswali yote
1. Huku ukitumia mifano, eleza kwa ufupi mitazamo mitano ya fasihi.
2. Orodhesha dhima tano za mtunzi wa kazi za fasihi.
3. Kwa kutumia mifano, toa maana ya maneno haya:
I. Uhakiki wa kazi za fasihi
II. Fasihi
III. Udhamini wa kazi za fasihi
IV. Tamathali za semi
4. A. Toa maana ya ushairi
B. Taja sifa nne za ushairi simulizi.

Sehemu B (Alama 60%)

Jibu maswali matatu, swali la nane ni la lazima.
5. “Washairi ni washauri wa jamii.” Thibitisha usemi huo kwa kutumia hoja nne kati ya diwani mbili ulizosoma.
6. “Dunia ni uwanja wa fujo.” Kwa kutumia riwaya mbili ulizosoma, thibitisha usemi huu ukitoa hoja nne kwa kila riwaya uliyosoma.
7. “Mapenzi ya kweli huondoa migogoro.” Fafanua ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja nne kwa kila kitabu katika tamthiliya mbili ulizosoma.
8. Soma matini ifuatayo kisha bainisha vipengele vya fani vilivyotumika.
Alisimama katikati ya jiji la Dar es Salaam. Jua kali… yeye mwenyewe alishangaa kwa nini jiji lilimkataa kiasi kile! Akiendelea kutafakari, jua likamchoma tena, ‘chooo’. Shati alilovaa, hapo zamani lilikuwa jeupe, lakini kwa sababu ya mapambano ya maisha, shati lilibadilika na  halikuwa na rangi ya kueleweka, lilibadilika na kuwa na rangi ya aina yake.
“This is impossible.” alisema kwa sauti. Mbwa aliyesimama jirani yake, akacheka, jamaa akakasirika, akarusha teke, mbwa akakwepa, akakimbia. Akasema tena kwa sauti, “Ukikosa pesa unadharauliwa mpaka na mbwa koko!” wapita njia wakamuunga mkono, “Ewaaaa!”
Zimwi likujualo halikuli likakwisha, jiji lilimfahamu, lakini sasa lilimtafuna na pengine Jamaa alibaki kipande kidogo ateketee. Alikonda kama uzi, alibaki mifupa mitupu. “Mjini, mjini, mjini...” aliendelea kuwaza kwa sauti.
Alikumbuka biashara yake ya kuuza pombe, biashara ilikwenda vizuri na alipata pesa nyingi wakati huo. Hata hivyo, biashara iliingia dosari baada ya kuibuka mchungaji mwenye upako. Mchungaji huyu alihubiri neno mpaka walevi wakaacha pombe, Jamaa akakosa wateja, akafirisika. Huo ukawa mwanzo wa maisha yake haya ya bahati mbaya!
Akisimama juani kwa muda mrefu, njaa iliongeza makali. Hakuwa hata na senti moja ya kununulia chakula, na tumbo lilitaka chakula. Ama kweli tumbo halina adabu. Basi akakumbuka maneno ya wahamasishaji, “unaweza kufanya chochote, unaweza… unaweza!” akikumbuka maneno hayo, akaokota jiwe kubwa, akaliweka katikati ya mikono yake kisha akasema kwa sauti, “Ewe jiwe… geuka mkate… geuka mkate mara moja, geuka mkate…”
Wapita njia walicheka, wakasikika wakisema, “Tayari dishi limeyumba!”
(Mwalimu Makoba: 2019)

Popular posts from this blog

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne