Mtihani wa Kiswahili 1 Kidato cha Sita 2020 1

Kabati la vitabu.

Maelekezo ya Kufanya Mtihani Ili Usahihishwe na Mwalimu:

1. Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
2. Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
3. Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21.
4. Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
5. Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili).
Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 25 05 66 (Daud Mhuli).
Muda: Saa 3

Sehemu A (Alama 20)

Ufahamu
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Soma kwa umakini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu kwa usahihi maswali yanayofuata:
Ni wanadamu wachache walio waaminifu. Hii ndiyo sababu pakawekwa vyombo mbalimbali vya kupambana na kundi la wengi wasio waaminifu. Kwa mfano, wasiowaaminifu katika ndoa, wanachombo cha kuwashikisha adabu kiitwacho talaka. Na wale wanaopora mali za watu husubiliwa kwa hamu na magereza.
Jambo kubwa linalosababisha kukosekana kwa uaminifu katika jamii ni umasikini kupita kipimo cha uvumilivu. Ni rahishi kwa mwanafunzi wa kike kutoa penzi kwa profesa ili apewe alama kwani asipofanya hivyo, atafelishwa masomo yake arudi nyumbani kuuendeleza umasikini.
Pia, si ajabu kumuona mke wa mtu akidanga. Pengine hakupewa pesa na mumewe hivyo kaamua kujiongeza ili watoto wasife njaa. Hata vijana wanaokaba katika vichochoro hawakupenda kazi hiyo, wametafuta namna ya kupata fedha kwa halali wakashindwa na kuamua kutumia njia hiyo ya mkato. Hata hivyo, vijana hawa wako hatarini kuchomwa moto wakiwa hai. Hatari kubwa hii.
Kwa hivyo, ili kuongeza kiwango cha uaminifu katika jamii yetu, ni sharti tuuondoe kwanza umasikini. Umasikini utaondoka kwa serikali kuweka sera safi zinazojali watu wote, nao watu wachape kazi na si kuishia maneno matupu.
Mkono mtupu haurambwi shehe!

Maswali

A. Andika kichwa cha habari hii.
B. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika habari hii:
I. Akidanga II. Vichochoro III. Talaka IV. Sera
C. Eleza mawazo makuu mawili ya mwandishi.
D. Kutokana na habari uliyosoma, taja chanzo kikuu cha kukosekana kwa uaminifu.
2. Fupisha habari uliyoisoma kwa maneno tisini.

Sehemu B (Alama 20)

Matumizi ya Sarufi na Utumizi wa Lugha
Jibu maswali mawili kutoka sehemu hii.
3. Fafanua mambo manne ya kuzingatia unapotumia lugha.
4. Bainisha mofimu na kisha taja kazi ya kila mofimu katika maneno yafuatayo:
A. Akijikingia B. Mchezaji C. Asiyekujua D. Mmeachiliana
5. A. Kwa kutumia mifano, fafanua maana ya istilahi zifuatazo:
I. Kielezi II. Kiwakilishi III. Kivumishi IV. Kitenzi
B. Kwa kutumia neno ‘zuri’ tunga sentensi mbili kwa kila aina za maneno yafuatayo:
I. Kielezi II. Kiwakilishi III. Kivumishi
6. Taja dhima tano za mofimu ‘ki’ katika sarufi kisha tunga sentensi mbili kwa kila dhima.

Sehemu C (Alama 20)

Utungaji
Jibu swali la saba.
7. Fafanua mambo sita muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa insha.

Sehemu D (Alama 20)

Maendeleo ya Kiswahili
Jibu swali moja kutoka sehemu hii.
8. Tumia hoja sita za kihistoria kuthibitisha kuwa Kiswahili ni kibantu.
9. Kwa kutumia hoja sita za kiisimu, thibitisha kuwa Kiswahili ni kibantu.

Sehemu E (Alama 20)

Tafsiri na Ukalimani
Jibu swali la 10.
10. Fafanua mambo sita ya kuzingatia wakati wa kutafsiri.

Popular posts from this blog

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne