Mwalimu Makoba Atunukiwa Cheti na Google | Digital Marketing

Cheti alichotunukiwa Mwalimu Makoba
Cheti alichotunukiwa Mwalimu Makoba na Kampuni ya Google
Anaandika Bugali S. Mongo | Mwandishi wa kujitegemea
Siku ya  tarehe 20/10/2019, Mwalimu Makoba ametunukiwa cheti na kampuni ya google wakishirikiana na vyuo vya IAB na The Open University ya London.
Cheti hiki kinamtambulisha Mwalimu Makoba kuwa mtaalamu wa biashara za mtandaoni yaani ‘digital marketing skills.’
Mwalimu Makoba amesema yeye ni mtanzania wa kwanza kupewa cheti na google! Hivyo anafuraha isiyo kifani kuvunja rekodi hiyo.
Pia Mwalimu Makoba amewaasa watu wengine wajifunze ‘digital marketing skills’ kwani mfumo wa biashara umebadilika kutokana na kuingia kwa intaneti.
“Hatuwezi kuweka matangazo ya biashara zetu katika nguzo za umeme ama kubandika katika nyumba za watu, njia hii haifanyi kazi tangu mwaka 98, sana utakosana na watu! Inasikitisha mtu ana biashara kubwa lakini ukiitafuta mtandaoni huipati.” alishauri Mwalimu Makoba.
Mwalimu Makoba ni Mwalimu mwenye shahada/degree kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Mbali na shahada ana vyeti na diploma zaidi ya sabini, alipoulizwa kuhusu wingi wa vyeti hivyo alisema,
“Ukiwa Mwalimu wa Walimu na Wanafunzi, unatakiwa uwe na maarifa mengi kuliko wanafunzi wako. Pia, kuhitimu kidato cha nne, cha sita na kupata shahada siyo mwisho wa kusoma, dunia inabadilika kila siku lazima uwe mpya. Upya huu utaupata kwa njia ya kusoma mambo yenye manufaa. Mwalimu Nyerere alisoma zaidi ya vitabu 8,000. Mwalimu ni mwanafunzi asiyehitimu. Soma!
Alimaliza mwalimu kisha tukaachana baada ya kuwa tumemaliza mazungumzo.
Bugali S. Mongo

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne