Kiswahili Online Examination Kidato cha Nne 1 2019

wanawake wakicheka
Endapo unataka kufanya mtihani huu ili usahihishwe na Mwalimu, zingatia mambo haya:
1. Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
2. Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
3. Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21. Bofya hapa kusoma maelekezo yote.

Muda: Saa 2.30

Maelekezo:

1. Jibu maswali yote isipokuwa kama imeelekezwa vingine katika maelekezo ya kipengele cha swali husika.

2. Andika jina lako katika kila ukurasa wa karatasi yako ya kujibia.

3. Mitihani isiyolipiwa, haitasahihishwa.

4. Kwa manufaa yako, usifanye udanganyifu.

Sehemu A (alama 10)

Ufahamu

1. Soma kwa makini kifungu cha habari kinachofuata kisha jibu maswali.

Walimwita Mzee Samawadi, naye bila hiyana aliafiki jina hilo. Mzee huyu ni mjuvi wa kijiji na hakuna njia asiyoifahamu. Mara nyingi alisaidia wasafiri ambao hawakufahamu njia sawa sawa, akawaelekeza hata wakatambua njia ya kwenda.
Samawadi alisifika kwa ule urumbi wa maneno. Kinywa chake kilipokosa cha kutafuna, kilifyatua maneno mengi. Hii ilimfanya apendwe na watu kwani jungu kuu halikosi ukoko.
Siku moja aliamka akiwa na hamu ya kwenda kuwinda, ni siku nyingi zimepita hajala nyama. Alijikokota yeye na dhana zake mpaka msituni tayari kuanza mawindo. Utu uzima dawa aliamini, kwa heri ama kwa shari lazima swala apatikane. “nimepata jiko nikiwa kijana mdogo, nitashindwa kumpata swala?” alijisemea taratibu.

Mzee alizurura msituni mule akitafuta mnyama, Hakumwona. Alizunguka kutwa nzima mwisho akagutuka na kuamua kurudi nyumbani. Alijisemea kimoyomoyo, anayeshindwa naye mwanamume.

Kizaazaa kilianza wakati wa kurejea. Hakuiona njia, alikuwa katikati ya msitu mkubwa wenye miti mingi mirefu. Alitafakari iwapo angeelekea mashariki, au kusini. Liwalo na liwe, akang’amua kuelekea mashariki.

Waswahili walisema njia ipo mdomoni, lakini hakumpata mtu wa kumuuliza njia ya kurejea. Aliamua kuhangaika hivyohivyo. Alitembea masaa mengi hata giza likawa limeingia. Hakuamini kwani yeye ndiye alikuwa mjuvi wa njia zote na sasa anapotea msituni namna ile. Ama kweli mganga hajigangi.

Kwa mbali aliona kitu kama kichuguu, aliamua kwenda kupumzika hapo, kukuche ili aendelee na safari yake ya kusaka njia ya kurejea nyumbani. Alikifikia kichuguu na
kujipumzisha hapo.

Akiwa kaegama katika kichuguu hicho, alisikia sauti za watu, “babu yenu hajarudi mpaka hivi sasa?” kusikia maneno hayo, akaamua kusogea. Loooh! Mbele alisimama
mjukuu wake aliyeitwa Chenja, kipilipili kimemkorea chenja kama utamu wa hadithi.

Ndipo mzee akagundua kuwa, alichoegama hakikuwa kichuguu bali ukuta wa nyumba yake. Alishangaa kuona kapotea lakini kafika nyumbani bila kujua. Aliahidi moyoni,
asubuhi ikifika, wakati wa kupata kifungua kinywa, atawasimulia watu wote mkasa uliompata.

Maswali

a. Kwa mujibu wa habari uliyosoma, eleza sababu iliyofanya Samawadi apendwe na watu.

b. Taja nahau moja iliyotumika katika habari hiyo.

c. Toa maana ya methali tatu zilizotumika katika habari hiyo.

d. Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma.

2. Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua miamoja (100)

Sehemu B (alama 25)

Sarufi na Utumizi wa Lugha

3. Fafanua dhana zifuatazo na kisha toa mfano mmoja kwa kila dhana uliyofafanua

a. Nomino

b. Kiwakilishi

c. Kivumishi

d. Kitenzi

e. Kielezi

4. Orodhesha njia nne za uundaji wa maneno. Toa mfano mmoja kwa kila njia.

Sehemu C (alama 10)

Uandishi

5. Elezea hatua za uandishi wa insha.

Sehemu D (alama 10)

Maendeleo ya Kiswahili
6. Onesha ushahidi wa kimsamiati na kimuundo unaothibitisha ubantu wa Kiswahili.

Sehemu E (alama 45)
Fasihi kwa ujumla
7. Ukitumia mifano kuntu, fafanua dhima sita za fasihi katika jamii.

8. “Mwanafunzi bora wa fasihi ni yule anayeitambua vyema taaluma ya ushairi.” Thibitisha kauli hii kwa kuhakiki vipengele vya fani katika diwani mbili ulizosoma.

9. “Bila fani hakuna riwaya.” Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kuhakiki vipengele vya fani katika riwaya mbili ulizosoma.

10. “Mwandishi bora wa tamthiliya, hukitumia kipengele cha fani vizuri ili aweze kueleweka.” Fafanua kauli hii kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma.

11. Utungaji wa mashairi unazidi kudorora siku hadi siku. Ili kuinusuru taaluma hii, ni lazima wanafunzi wafundishwe mashuleni namna ya kutunga mashairi.

a. Fafanua kanuni tatu au zaidi za utungaji wa mashairi

b. Tunga shairi la kimapokeo kuhusu umuhimu wa mitandao ya kijamii.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne