Usanii Unavyojitokeza Kwenye Sala Tabano na Hotuba

sherehe za matambiko
Sala tabano ni sala ambazo hufanywa ili kumtakia mgonjwa nafuu. Eneo la sala hizi laweza kuwa kwa mganga wa kienyeji au mganga mwenyewe anaweza kumtembelea mgonjwa.
Hotuba ni maelezo maalumu yanayotolewa mbele za watu na mtu mmoja. Kwa mfano mbunge anaweza akatoa hotuba kwa watu wake akiwaeleza jinsi alivyotatua shida zao wakati alipokuwa bungeni na bila shaka huenda akawaomba wamchague tena ili aendelee kuchapa kazi.
Kwanza nitaonyesha usanii katika sala tabano, na kisha nitazungumza kwa ujumla, yaani usanii katika sala tabano na usanii katika hotuba.
Usanii katika sala tabano
- Matumizi ya nyimbo. Sala tabano hutumia nyimbo maalumu. Mganga na msaidizi wake huimba nyimbo zinazoeleweka na zile zisizoeleweka.
- Matumizi ya lugha maalumu. Katika sala tabano lugha ya pekee hutumiwa. Mara nyingi maneno katika lugha hii huwa hayaeleweki vizuri.
Usanii katika sala tabano na hotuba
- Sala tabano na hotuba hushirikisha hadhira. Watu hutakiwa kuitikia maneno fulani ama kurudia kile kinachosemwa. katika hotuba, mzungumzaji huweza kuuliza, tuko pamoja na hadhira nao wakaitikia “ndiyooo.”
- Sala tabano na hotuba zina eneo maalumu la kufanyikia. Sala tabano huweza kufanyikia nyumbani kwa mganga au mahali popote maalumu. Hotuba nayo huweza kufanyika uwanjani au mahali popote palipoandaliwa kwa ajili hiyo.
Mwanafunzi wangu mmoja, alitaka kujua kuhusu muundo. Nami nikajibu,
“Muundo ni mpangilio wa visa na matukio. Hotuba huwa katika mpangilio maalumu yaani huanza utangulizi, kiini kisha likafuata hitimisho. katika sala tabano maombi hufanywa kwa mpangilio maalumu.”
Baada ya jibu langu, alipata dukuduku akasema,
“Tabano si muundo changamano? Kwa sababu pind mgonjwa/ mwele afikapo kwa mganga ,mganga anaweza akamweleza matatizo yake kabla mwele hajaeleza.”
Nami nikajibu,
“Kama nilivyosema awali, taaluma ya chuo ina majibu kinzani kulingana na marejeo uliyosoma au kile unachoamini wewe. Hivyo unachokisema kiko sawa kulingana na marejeo yako. Je kila mganga ana uwezo wa kuyajua matatizo ya mgonjwa kabla ya kuelezwa? Ukweli ni kwamba hakuna awezaye kujua lililomsibu mtu fulani bila yeye mwenyewe kueleza. Habari ya mganga kuyajua matatizo ya mtu ni uongo uliotazamwa kwa jicho zuri.”

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie