Mtihani wa Kiswahili 2 kwa Wanafunzi wa Kidato cha Sita 1

picha ya kuvutia

Endapo unataka kufanya mtihani huu ili usahihishwe na Mwalimu, zingatia mambo haya:
1. Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
2. Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
3. Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21.
4. Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
5. Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili).
Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 25 05 66 (Daud Makoba)
“Kwa kuwa lengo la mtihani huu ni kutaka kujua uwezo na mapungufu ya mwanafunzi ili aweze kupewa mbinu mbadala za kumsaidia kufaulu mtihani wake wa mwisho, kuangalizia majibu hakuna faida yoyote kwani lengo la mtihani si kubaini nani atakuwa wa kwanza na yupi atakuwa wa mwisho!”
Sasa fanya mtihani wako…
Tumia saa 3
Maelekezo:
Fanya swali moja kutoka kila kipengele
Sehemu A (Alama 20)
Fasihi kwa Ujumla
1. Kwa kutumia mifano, elezea tofauti nne kati ya fasihi ya Kiswahili na Fasihi kwa lugha ya Kiswahili.
2. Lengo la hadhira ni kuipa uhai kazi ya fasihi simulizi. Elezea dhima tatu za hadhira katika utanzu wa hadithi na zima mbili za hadhira katika utanzu wa vitendawili
Sehemu B (Alama 20%)
Ushairi
3. “Uongozi mbovu ni kikwazo kwa jamii katika kujipatia maisha bora.” Jadili uhalisia wa kauli hii kwa kutoa mifano minne kwa kila kitabu kutoka katika diwani mbili ulizosoma.
4. “ushairi ni msingi wa maneno yenye hekima kwa jamii ya leo.” thibitisha usemi huo kwa kutoa hoja nne kwa kila diwani kutoka katika diwani mbili ulizosoma.
Sehemu C (Alama 20)
Riwaya
5. “mitazamo ya waandishi wa kazi za fasihi hutofautiana kati ya mwandishi mmoja na mwingine.” Kwa kutumia hoja nne kwa kila kitabu, bainisha mitazamo ya waandishi wawili wa kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.
6. “Dunia ni tambara mbovu.” Thibitisha usemi huu kwa kutoa hoja nne kwa kila kitabu kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.
Sehemu D (Alama 20)
Tamthiliya
7. “Mapenzi ya kweli ni jawabu la migogoro mingi katika jamii.” fafanua ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja nne kwa kila kitabu kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma.
8. Majibizano ni kipengele muhimu katika kuumba na kubeba wazo la mwandishi. Kwa kutumia hoja tatu kwa kila kitabu, onesha jinsi majibizano yalivyotumiwa na waandishi kujenga na kupendezesha kazi zao kupitia tamthiliya mbili ulizosoma.
Sehemu E (Alama 20)
Usanifu wa maandishi
9. Soma matini ifuatayo kisha bainisha vipengele vya fani vilivyotumika.
Majambazi wale walitaka fedha. Kwanza walitaka kuchukua fedha kwa wahudumu waliokuwa wakiuza vinywaji, kisha warudi kwa watu kila mmoja aweke kiasi alichokuwa nacho. Mako alilitambua hilo, akatabasamu kama kitoto cha mamba.
Mako alimwomba Lightness atulie, kisha akatambaa taratibu bila kuonekana mpaka sehemu palipouzwa vinywaji, alipofika, akatega pale mithili ya chatu mwenye njaa.
Jambazi aliyekuwa na siraha, akaanza kutembea kuelekea sehemu palipouzwa vinywaji ili kuchukua fedha, alipofika mahali pa kuingilia, Mako akamvuta miguu yake na kumwangusha chini, haraka akampokonya bastola yake. Mwenzake kule mbele akataka kukimbia, Mako akamtandika risasi ya mguu akadondoka chini akigugumia maumivu. Watu walipoona Mako anapambana na mpambano kauweza, wakawakamata wale majambazi wasio na bahati wakitaka kuwashushia kipigo. Mako kuona hivyo akanena, “Jamani, muda uliobaki ni kidogo sana, tukianza kuwapiga hawa, asubuhi itafika hatujacheza mziki, mimi naomba mabaunsa watusaidie kuwapeleka polisi waharifu hawa. Sisi tuendelee kucheza muziki.
Watu wakashangilia kukubaliana na hoja ya Mako, muziki ukawashwa, Lightness akasogea alipo Mako, nyonga ikaendelea kuzungushwa. Hata hivyo watu walicheza mbali kidogo na Mako, walimwogopa, ni binti mmoja tu ambaye hakumhofia Mako, Lightness!

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne