Mtihani wa Kiswahili 1 kwa Wanafunzi wa Kidato cha Sita 1

mtu akitumia simu

Endapo unataka kufanya mtihani huu ili usahihishwe na Mwalimu, zingatia mambo haya:
1. Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
2. Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
3. Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21.
4. Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
5. Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili).
Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 25 05 66 (Daud Makoba)
“Kwa kuwa lengo la mtihani huu ni kutaka kujua uwezo na mapungufu ya mwanafunzi ili aweze kupewa mbinu mbadala za kumsaidia kufaulu mtihani wake wa mwisho, kuangalizia majibu hakuna faida yoyote kwani lengo la mtihani si kubaini nani atakuwa wa kwanza na yupi atakuwa wa mwisho!”
Sasa fanya mtihani wako…
Tumia saa 3
Sehemu A (Alama 20)
Ufahamu
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu kwa usahihi maswali yanayofuata.
Kipindi cha kuanzia mwaka 1930 hadi 1938 kilikuwa muhimu sana kwa historia na usanifishaji wa lugha Kiswahili. Mambo mbalimbali yalifanyika ili kuhakikisha kuwa kiswahili kinastawi na kushamiri. Kuundwa kwa kamati maalumu ya kushughulikia lugha ya Kiswahili katika nchi za Afrika Mashariki, ilikuwa hatua muhimu sana katika kukikuza na kukieneza Kiswahili.
Kazi za kamati ya lugha ya Afrika Mashariki zilikuwa nyingi kama vile, kusanifisha otografia itakayotuika kwa watumiaji wote wa Kiswahili, kuandaaa kamusi mbalimbali, kutoa hamasa kwa waandishi wachanga wanaotumia lugha ya Kiswahili katika kuandika kazi zao, kusahihisha lugha katika vitabu vilivyokuwa vinatumika kufundishia shuleni na kufanya tafiti mbalimbali za lugha ya Kiswahili.
Kamati ya lugha ya Afrika Mashariki ilifanya kazi chini ya usimamizi wa utawala wa mwingereza; kazi za kamati zilipamba moto huku tafiti mbalimbali kuhusu lahaja za kiswahili zikiendelea kufanyika. Tafiti hizo zilizaa matunda na hatiamye ikaonekana ni vizuri kuchagu lahaja moja na kuisanifisha ili iwe msingi wsa JKiswahili sanifu.
“Mungu hamtupi mja wake,” sudi iliangukia kwa lahaja ya kiunguja na ilichaguliwa kuwa lahaja ya Kiswahili sanifu. Watumiaji wa lahaja zingine walikuwa na inda baada ya lahaja ya kiunguja kutangazwa kuwa msingi wa usanifishaji wa Kiswahili. Kamati haikufanya ajizi, ilianza mara moja kusanifisha lugha ya Kiswahili. Kiswahli sanifu tukitumiacho leo ni matunda ya kazi ya utawala wa mwingereza katika usanifishaji wa lahaja ya kiunguja.
Kwa ujumla tunaweza kusema kati ya wakoloni wote, wakoloni wa kiingereza ndio waliofanya kazi kubwa katika kuikuza na kuiendeleza lugha ya Kiswahili. Kupitia sera na mfumo wa utawala wa wakati huo walifanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa Kiswahili kinakua na kuenea kati nchi za Afrika Mashariki.
Maswali
A. Andika kichwa cha habari hii kwa maneno matatu.
B. Toa maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika habari uliyosoma.
I. Usanifishaji
II. Zilipamba moto
III. Lahaja
IV. Kiswahili sanifu
V. Sudi
C. Usemi, “Mungu hamtupi mja wake,: una maana gani?
D. Mwandishi anauelezeaje mchango wa wakoloni wa kiingereza katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili?
2. Fupisha habari uliyosoma kwa maneno mia moja.
Sehemu B (Alama 20)
Matumizi ya Sarufi na Utumizi wa Lugha
Jibu maswali mawili kutoka sehemu hii.
3. Fafanua maana ya dhana za sarufi ya Kiswahili zifuatazo:
A. Ngeli za majina
B. Mofimu
C. Kirai
D. Sentensi
E. Mzizi
4. Kwa kutumia mifano kutoka katika lugha ya Kiswahili, toa hoja tano kubainisha tofauti kati ya mofimu tegemezi na silabi.
5. Kwa nini ni muhimu kuzingatia uhusiano baina ya wahusika wakati wa kutumia lugha? Toa hoja tano.
6. Toa maana tano za neno pasi na kwa kila maana tunga sentensi moja.
Sehemu C (Alama 20)
Utungaji
Jibu swali la saba
7. Jifanye wewe ni afisa habari wa shirika la ndege Tanzania, andika tangazo kwa abiria kuhusu katizo la usafiri wa ndege namba TY JET 343 iliyokuwa ifanye safari yake toka Songea kwenda Zanzibar siku ya Ijumaa tarehe 25/5/2018 saa 12 asubuhi, kuwa safari hiyo itafanyika Jumapili tarehe 27/05/2018 saa nane mchana. Mabadiliko haya yanatokana na kuchafuka kwa hali ya hewaa angani. Jina la mtoa tangazo liwe kudura Riziki. 
Sehemu D (Alama 20)
Maendeleo ya Kiswahili
Jibu swali moja kutoka sehemu hii
8. Jadili changamoto sita zinazoikabili lughaya Kiswahili nchini Tanzania.
9. Fafanua sababu sita zilizochangia lugha ya Kiswahili isikue na kuenea kwa kiwango kikubwa nchini Uganda kabla ya uhuru.
Sehemu E (Alama 20)
Tafsiri na Ukalimani
Jibu swali la 10
10. Katika Tanzania ya leo taaluma ya tafsiri haiwezi kuepukika. Kwa kutumia hoja tano, thibitisha kauli hiyo.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne