Maswali Mbalimbali ya Kiswahili na Majibu yake


Nimekuwa nikiulizwa maswali mbalimbali na wanafunzi, nami nipatapo muda, huyajibu maswali hayo. Kwa kuwa ni maswali yanayoulizwa sana, pengine hata wewe ukawa unatafuta majibu yake. Twende pamoja.

Baadhi ya majibu yamejibiwa kwa lugha ya mkato ili kuokoa muda!

1. Vigano ni nini? tunga vigano kwa kutumia methali isemayo "umdhaniaye ndiye kumbe siye."

Vigano ni hadithi fupifupi zinazosimuliwa kwa lengo la kueleza makosa au maovu ya watu fulani ili kutoa maadili mema yanayofaa kwa wanajamii.

Masimulizi ya vigano mara nyingi hutumia methali kama msingi wake wa maadili. Methali hiyo ndiyo hujengewa masimulizi yanayolenga kumwonya mwanajamii anayetenda kinyume na maadili ya jamii yake.

UMDHANIAYE NDIYE KUMBE SIYE

Mzee Magani alimwamini sana mke wake, hakudhani siku moja angekuja kumfanyia unyama. Alimpenda na kumjali sana, alisahau msemo wa wahenga kuwa, umdhaniaye ndiye kumbe siye.

Siku moja akiwa katika harakati za maisha za kila siku, alikumbuka kuwa amesahau pochi yake nyumbani, akaamua kurejea haraka sana.

Hakuamini alichokiona alipofika nyumbani, mkewe aliyempenda alikuwa kalala na mwanaume mwingine. Moyo ulimuuma sana Mzee Magani.

Kweli umdhaniaye ndiye kumbe siye.

2. Tunga shairi la kimapokeo lenye beti nne kuhusu rafiki yako anaehamia shule nyingine.

NITAKUKUMBUKA RAFIKI

Mehama mapema sana, rafiki yangu kipenzi,
Nitakukumbuka mana, ulinifanya mjenzi,
Na mimi sina namna, lakini nitakuenzi,
Huko unakohamia, nina kutakia heri.

Sichoki kukuambia, kwa hapa kwetu shuleni,
Na wote tulitembea, furaha tele pomoni,
Huzuni meniachia, machozi tele machoni,
Huko ulikohamia, ninakutakia heri.

Uendako soma sana, uniwakilishe vyema,
Fanya yote yalo mana, heshimu baba na mama,
Masomo usije kana, elimu ifanye hema,
Huko ulikohamia, ninakutakia heri.

malizia ubeti wa mwisho kwa kanuni hizo 👆🏽

3. Tunga tamthiliya fupi kuhusu umuhimu wa elimu kwa vijana wa Tanzania ya leo tamthiliya hiyo isipungue maneno mia tatu


UMUHIMU WA ELIMU KWA VIJANA

(Jukwaani anaingia Afisa elimu wa wilaya, anafuatiwa na watu wake kwa nyuma)
AFISA ELIMU: Wanakijiji oyeeee!
WANAKIJIJI: Oyeeee!
AFISA ELIMU: Ndugu zangu, awali ya yote niwashukuru sana kwa kujitokeza kuja mahali hapa, kusema kweli nataka niwape mawili matatu kuhusu umuhimu wa elimu. Mko tayari kunisikiliza?
WANAKIJIJI: Ndiyooooh!
AFISA ELIMU:  Elimu ni muhimu sana ndugu zangu, nimekerwa sana na tabia yenu ya kuwaachisha watoto shule ili waolewa na wale wa kiume ili wachunge ng'ombe. Ndugu zangu, hamuujui umuhimu wa elimu?
MLEVI: Waambie, hasa Mzee Jimbi kazidi kuoa watoto wadogo... (Kabla hajaendelea, Jimbi anamkata kibao na kumkarisha chini kwa nguvu)
AFISA ELIMU: Bila elimu hakuna biashara, hakuna usafiri, hakuna maendeleo, hata chakula kitapatikana kwa... (Anakatisha hotuba yake, anatazama juu anaona wingu zito limetanda, mvua kubwa inaanza kunyesha, watu wote wanasambaa na yeye anaelekea kwenye gari.)

Huu ni mfano wa namna tamthiliya ilivyo. Tamthiliya ndefu zaidi inaweza kuandikwa. Ili utimize maneno 300, hakikisha tamthiliya yako ina kurasa mbili.

4. Taja Athari ya Waarabu Katika Lugha ya Kiswahili

1. Athari katika msamiati wa lugha ya kiswahili

2. Athari katika matamshi

3. Athari katika maandishi

4. Athari katika ushairi wa kiswahili. Ujio wa mashairi yenye urari wa vina na mizani.

5. Jadili jinsi majina ya Riwaya mbili yalivyo sadifu yaliyomo

Watoto wa Maman'tiliye

1. Ndani ya kitabu tunawaona watoto wa mamantiliye ambao ni Zita na Peter.

2. Pia, ndani ya kitabu kuna mhusika ambaye ndiye Mamantiliye. Mama huyu anafanya kazi ya kuuza chakula.

3. Pia, maisha anayoishi Mamantiliye ni  ya dhiki kama walivyo mamantiliye wengi.

Takadini

1. Maana ya neno Takadini ni sisi Tumekosa nini? Takadini anataka kuuwawa na jamii yake bila kosa lolote.

2. Nhamo anamchukia Takadini bila sababu yoyote ya msingi.

3. Pia, Halikuwa kosa la Takadini kuzaliwa mlemavu, hata hivyo watu walimbagua na kumnyanyasa. Mfano, baba yake Shingai, hakutaka Takadini amwoe mwanaye.

6. Toa sababu kwa nini kiswahili kilienea zaidi nchini  Tanzania  kuliko Kenya na Uganda

i. Biashara kwa Kenya na Uganda shughuli za kibiashara zilizuiwa na wanyam mfano mbuga ya TSavo tofaut na Tanzania biashara haikuzuiwa na wanyama wakali.

ii. Elimu katika kenya na Uganda lugha za makabila zilipewa nafas sana katika kutolea elimu mfano Kikuyu, kiganda tofauti na Tanzania lugha ya kiswahili ilitumika kutolea elimu.

iii. Utawala katika utawala Tanzania shughuli zote zilifanywa kwa lugha ya kiswahili tofauti Kenya na Uganda lugha za makbila zilipewa nafasi Sana katika kukikuza kiswahili.

7. Eleza matukio saba muhimu yaliyofanywa na serikali za tanganyika na zanzibar katika harakati za kusanifisha lugha ya kiswahili kabla ya miaka ya 1960

Tukio la kwanza  mwak 1925,gavana aliitisha mkutano wa kwanza dsm lengo ni kuchagua lugh moja itakayotumiw na nch nne. 

Tukio la pil mwak 1928,waliteuwa lahaj ya kiunguja kuw lugha ya usanifixhj mktno huo walikaa mombaxa kenya.

tukio la tatu mwk 1930,waliund kamt ya usanifixhaj kiswhl (swahil comittee).

tukio la nne mwk 1948, kuundwa kwa shirika la upitiaj na uchpishaj wa mswaada ambao uliitwa (the east africa literature bereau).

tukio la tano mwk 1952, kuiweka kamat ya kisw chin ya chuo cha afrk maxhark cha uchunguz wa jamii.

tukio la sita,kuundwa kwa vyombo vya habar kama vile magazet,yaliitw mamboleo,habar leo,na baraza pia redio kam vile saut ya dxm.

 Tukio la saba mwk 1959,cham cha uxanfishaj (ukuta)kiliundwa lengo likiwa ni kuhamaxisha vijana wnyj waliotk kuw mafnd wa lugha ya ksw

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie