TAMTHILIYA; KILIO CHETU MWANDISHI; MEDICAL AID FOUNDATION MCHAPISHAJI; TANZANIA PUBLISHING HOUSE MWAKA; 1995 JINA LA MHAKIKI; Mwalimu Daud Makoba Kilio chetu ni tamthiliya inayovunja ukimya uliotawala miongoni mwa jamii katika kutatua matatizo makubwa ambayo chimbuko lake ni mahusiano ya kijinsia. Katika tamthiliya hii vijana wanatoa sauti ya jitimai iliyojaa sononeko na shutuma dhidi ya wazazi, walezi na viongozi ambao wanafumbia macho suala hili nyeti. Ndiyo maana tamthiliya hii inasisitiza sana haja ya kuwapa vijana elimu juu ya mahusiano ya kijinsia badala ya hofu na vitisho ambavyo vimedhihirika kupitia hali halisi ya kuwa vimeshindwa. FANI MUUNDO Tamthiliya hii imetumia muundo wa moja kwa moja. Inaanza kwa kutuonesha wazazi wakibishana juu ya kutoa elimu ya jinsia na mahusiano. Mwisho Joti mtoto ambaye hakupatiwa elimu hiyo anampa mimba mtoto mwenzake Suzi. Baadae Joti anakufa kwa UKIMWI. Pia tamthiliya hii imegawanywa katika sehemu sita. sehemu y
Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi. CV au wasifu ni kitu cha lazima kwa yeyote anayeomba kazi. Watu wengi wanaokosa kazi, tatizo huwa siyo wao, bali tatizo huwa ni CV zao. Kumekuwa na makosa mengi katika uandishi wa CV jambo ambalo limesababisha watafuta kazi wengi kushindwa kuitwa kwenye usaili. Makala hii itakueleza namna sahihi ya kuandika CV, utaitwa katika ‘interview’ nyingi endapo utaandika CV sahihi. Tena nakukumbusha, kila taaluma ina aina yake ya CV, CV ya rubani haifanani na CV ya injinia. Vivyo hivyo, CV ya mpishi haifananani na CV ya Mwalimu. Pia nakukumbusha usome jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi , kwani CV huenda pamoja na barua ya maombi ya kazi. CV Bora ni Ipi? Ukurasa Mmoja au Kurasa mbili hadi tatu? CV bora ni ile yenye kurasa mbili hadi tatu. Watu wengi wanapojifunza namna ya kuandika CV, wamekuwa wakiona CV zenye ukurasa
Hotuba ni maelezo ambayo hutolewa na mtu mbele ya watu kuhusu mada fulani. MUUNDO WA HOTUBA - Mwanzo. Huu huambatana na salamu. - Utangulizi. Hutaja watu na kuwatambulisha kulingana na vyeo vyao. - Kati. Hiki ni kiini cha hotuba. Mawazo yote makuu hukaa hapa. - Mwisho. Muhtasari wa yale yaliyoelezwa. Pia, msemaji hupata nafasi ya kuaga na kushukuru. Sasa tazama mfano halisi wa hotuba ambao umeandikwa kama majibu ya swali la nane mtihani wa kumaliza kidato cha nne 2010. Eleza tofauti iliyopo kati ya hotuba na risala. Andika hotuba kuhusu “Maji ni Uhai.” Kwa kuwa mjadala wetu ni hotuba , risala haitazungumziwa, bali nitajikita katika kuonyesha mfano wa hotuba. MAJI NI UHAI Wanakijiji oyeeeeeeh! Ndugu Mwenyekiti wa Kijiji, ndugu Katibu wa Kijiji, Ndugu Wanakijiji wote mabibi na mabwana. Ninafurahi kusimama mbele yenu na kuzungumza. Nikiwa kama mwanaharakati wa muda mrefu wa utunzaji wa vyanzo vya maji, leo nasimama tena kuwaeleza na kuuthibiti