Mtihani wa Kiswahili Kidato cha Tatu Annual | Past Papers

Mtihani wa Kiswahili Kidato cha Tatu Annual| Past Papers
Photo Credit: ZanziNews
SEHEMU A (alama 10)
1.   Soma kifungu hiki cha habari kisha jibu maswali yanayofuata:
ANA wajukuu wanne, umri wake ni miaka 70, na kila mmoja hushangazwa na muonekano wake! Ni bibi asiye mzee.  Ajabu kubwa.
Siri pekee inayomfanya awe na muonekano huo ni aina ya vyakula anavyokula na kuzingatia mazoezi ya kutosha. Anazingatia anachoweka mdomoni na miguu yake haiishi kutembea.
Bibi huyu, anayetokea Perth, Australia, wakati alipokuwa na umri wa miaka 40 alitahadharishwa na madaktari kuwa endapo angeshindwa kubadili mtindo wa maisha, punde angeugua maradhi ya kisukari. Ili  kuokoa maisha yake, akaamua kuvipa kisogo vinono vyote, na huo ndiyo ukawa mwanzo wa maisha mapya. Ni mwanzo huu unafanya tumzungumzie! Siri ya Bi Carolyn Hartz kuonekana kama binti mdogo.
Ukiachilia mbali vyakula sahihi anavyokula, hulala kwa muda wa saa saba, kujishughulisha na kazi zake binafsi siku nzima, na kama ilivyo asili ya wanawake wengine, hutumia muda kiasi kujipamba. Kipo cha kujifunza kutoka kwa bibi huyu.
i.             Kipi kinafaa kuwa kichwa cha habari hii?
ii.            Taja siri pekee inayomfanya Bi Caroly Hartz kuwa na mwonekano alionao sasa?
iii.           Toa maana ya neno kuvipa kisogo vinono vyote.
iv.          Kwa mujibu wa kifungu hiki cha habari, unafikiri ni ipi njia sahihi ya kufukuza maradhi?
v.           “Kipo cha kujifunza kutoka kwa bibi huyu.” Taja mafunzo manne uliyoyapata.
2.   Fupisha habari hiyo kwa maneno yasiyozidi 60

SEHEMU B (alama 30)

3.   Toa maana ya upatanishi wa kisarufi. Weka mifano minne.
4.   Ni ipi tofauti ya kirai na kishazi? Kwa kuzingatia mifano, toa tofauti mbili kwa kila moja.
5.   Kwa kutumia kigezo cha kimuundo, taja aina tatu za sentensi. Toa mifano kwa kila aina.

SEHEMU C (alama 20)

6.   Wewe ni mfanyabiashara wa vipuri vya magari. Andika tangazo la biashara yako litakalochapwa katika gazeti la MWENDAKWAO litokalo kila Jumamosi.
7.   Andika barua ya maombi ya kazi ya ulinzi katika mgodi wa Buzwagi. Tumia ubunifu wako kuweka jina na anuani ya unayemwandikia.

SEHEMU D (alama 10)

8.   Thibitisha mfanano wa kimsamiati wa Kiswahili na lugha nyingine za kibantu

SEHEMU E (Alama 30)

9.   Tunga ngonjera kuhusu kisa kisemacho, MJINI NI BORA KULIKO KIJIJINI.
10.       Tumia riwaya ya Watoto wa Maman’tilie kuthibitisha jinsi watu wazima wanavyoshindwa kutimiza wajibu wao katika jamii.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne