Mtihani wa Kiswahili 2 kwa Kidato cha Sita| Pre Necta
![]() |
Photo Credit: nacelesl |
Maelekezo
1. Mtihani huu una maswali 9 yaliyogawanywa katika sehemu
A, B, C, D, E.
2. Jibu maswali 5 kwa kuchagua swali moja kutoka kila
sehemu.
3. Kila swali lina alama 20.
4. Andika jina lako katika karatasi ya kujibia.
JINSI YA KUUFANYA MTIHANI HUU
Mtu yeyote na kokote aliko
anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
Fanya mtihani huu kwa kutumia
aina yoyote ya karatasi.
Ukimaliza, piga picha karatasi
hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba - 0754 89 53 21.
Subiri mtihani wako usahihishwe,
Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
Gharama ya mtihani huu ni
shilingi 2,000 (elfu mbili) tu.
Namba za malipo ni: M – Pesa 0754
89 53 21 na Tigo pesa 0653 25 05 66
“Kwa kuwa lengo la mtihani huu ni
kutaka kujua uwezo na mapungufu ya mwanafunzi ili aweze kupewa mbinu mbadala za
kumsaidia kufaulu mtihani wake wa mwisho, kuangalizia majibu hakuna faida
yoyote kwani lengo la mtihani si kubaini nani atakuwa wa kwanza na yupi atakuwa
wa mwisho!”
Daud Makoba – Mwalimu Makoba –
Mwalimu wa Waalimu.
Unataka kufanya mtihani huu na
hujaelewa taratibu zake? Wasiliana na Mwalimu Makoba kwa 0754 89 53 21.
Sasa fanya mtihani wako.
SEHEMU A (Alama 20)
FASIHI KWA UJUMLA
1. “Fasihi ni chombo cha moto kwa watawala”. Jadili
ukweli wa kauli hii kwa kuzingatia udhibiti wa kazi mbalimbali za fasihi kabla
na baada ya kupata uhuru mpaka hivi sasa.
2. Onyesha jinsi sayansi na teknolojia inavyoua fasihi simulizi.
SEHEMU B (Alama 20)
USHAIRI
3. “Ni ukweli usiopingika kuwa, wasanii ni chachu ya
maendeleo katika jamii.” Tumia hoja tatu kwa kila diwani kujadili ukweli wa
hoja hiyo.
4. “Ushairi wa kimapokeo hutofautiana na ushairi wa
kisasa kifani.” Thibitisha hoja hii kwa kutumia diwani mbili ulizosoma.
SEHEMU C (Alama 20)
RIWAYA
5. Eleza jinsi mapenzi yalivyowatesa wahusika wa riwaya
mbili ulizosoma.
6. Jadili wahusika wawili kwa kila kitabu ambao unaamini
hawatakiwi kuigwa na jamii na taja sababu zenye mashiko kuthibitisha madai
yako.
SEHEMU D (Alama 20)
TAMTHILIYA
7. “Tamthiliya ni mchezo wa kuigizwa na kuachwa jukwaani.
Kuandikwa ili kusomwa na vizazi vya sasa na vijavyo ni kazi bure.” Jadili uongo
na uzandiki wa kauli hiyo.
8. Wakati na matukio yanayotokea katika jamii huakisi
ujenzi wa tamthiliya. Jadili rai hiyo kwa kutoa hoja tatu kwa kila tamthiliya.
SEHEMU E (Alama 20)
USANIFU WA MAANDISHI
9. Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali
yatakayofuata.
Ninashuka kifuani, kwenye matuta natua,
Wanaume huyatamani, hupenda kuyasugua,
Yadumishe mafichoni, sipende kuyafungua,
Ukisharudi chumbani, kaanze
kuyakagua.
Wanaume wakiona,hutamani kuyagusa,
Kwa hoja na kubishana, wakivizia ruhusa,
Ukijilegeza mwana, wanafaidi kabisa,
Ujanja wako wa jana, watauyeyusha
hasa.
Tazama yalivyotuna, au yalivyochongoka,
Huo ndiyo usichana, kama hayajadondoka,
Uwachunge wavulana, wasije wakayateka
Daima sema hapana, MATITI SIYO
SADAKA.
Maswali
a. Eleza dhima tatu za shairi hili.
b. Mshairi ana maana gani katika maandishi ya herufi
kubwa mwishoni mwa shairi.
c. Eleza matumizi ya takriri vina katika shairi.
d. Kipi kinafaa kuwa kichwa cha shairi hili?
e. Mshairi anampenda binti yake? Kama jibu ni ndiyo, toa
sababu.
Mwalimu Makoba 0754 89 53 21/ 0653 25 05 66