Watanzania Wanazungumza Kiswahili au Viswahili?

Watanzania Wanazungumza Kiswahili au Viswahili?

Ni swali zuri lenye mifano halisi. Hata hivyo, majibu yake hayapo katika upande mmoja, hivyo basi, Watanzania tunazungumza Viswahili na Kiswahili kwa pamoja.
Viswahili ni lugha inayotoka katika kiswahili ambayo ama hakika huwa ni kiswahili kilichokosewa. Makosa haya yaweza kuwa ya kukusudiwa kwa maana ya kupangwa na mzungumzaji au yanaweza kuwa kinyume chake. Kwa mfano: mzungumzaji wa lugha anaposema, “mtaani hakukaliki, mamwera wanatembea na tenga lao kila chocho!” lugha hii si Kiswahili rasmi, hivyo moja kwa moja inaingia katika Viswahili.

Kuhusu Kiswahili

- hii ndiyo lugha ya taifa na lugha rasmi. Hivyo mazungumzo ya kiofisi na shuleni mara nyingi hutumia Kiswahili kilichofasaha. Kwa kuongezea zaidi, lugha itumikayo katika vyombo vya habari kama radio, televisheni na magazeti huwa ni lugha rasmi. Hata hivyo, si mara zote kwamba vyombo vya habari hutumia lugha rasmi. Kuna wakati makosa ya kupangwa na yale ya bahati mbaya huweza kutokea.

Kuhusu Viswahili

Zipo sababu nyingi zinazowafanya watu wazungumze viswahili badala ya Kiswahili.  watu walioathiriwa na lugha mama hujikuta wakizungumza viswahili. Kwa mfano, mnyakyusa anaposema, "hifi ni fiatu fyangu.
- Vijana wahuni katika vijiwe hutumia viswahili. Maneno kama, 'mingo', 'manzi', 'shega', 'shwanga', 'shemela', n.k
Sababu nyingine inayowafanya wazungumzaji wa lugha wazungumze Viswahili ni kutokujua hasa maneno sahihi ya lugha hii. Wapo watu waliozaliwa katika maeneo ambayo kwa muda mwingi Kiswahili kizungumzwacho huko huwa ni kile kilichojaa misimu ya eneo hilo. Watu kama hawa hudhani wanazungumza lugha sahihi kumbe sivyo!
Viswahili vinashusha hadhi na heshima ya lugha ya Kiswahili. Siku za hivi karibuni, mitandao ya kijamii inasaidia kusambaa kwa viswahili hivyo. Kwa bahati mbaya sana, hata vyombo vya habari navyo vinachangia katika uungaji mkono wa Viswahili. Ni lazima sasa elimu ya kutosha itolewe juu ya faida na umuhimu wa uzungumzaji wa lugha sahihi.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu