Sitasahau Nilipolala na Mwanamke Juu ya Kaburi (28)| Riwaya

Sitasahau Nilipolala na Mwanamke Juu ya Kaburi (28)| Riwaya

Nikiwa nimekaa katika kiti kimojawapo miongoni mwa viti vile vinne, mlango ulifunguliwa. Aliyefungua mlango ule ndiye aliyeingia. Alikuwa msichana nisiyeweza kutambua umri wake. Hata hivyo, aliumbwa vyema akaumbika. Kiunoni alivaa ngozi fupi hivyo nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuuona uzuri wa mapaja yake ya rangi ya kunde. Nilipoyaona manyoya laini ya kike chini kidogo ya kitovu chake, damu ilikwenda kasi na kunifanya nisahau kabisa kama nilikuwa mateka.
Alikuwa na sura ndogo tamu, nyusi nyingi na midomo minene, kifuani paliinama na hapakuwa na mpango wa kudondoka. Fahari ya macho ni kwamba, kifuani hakufunga chochote! Mkono wa kushoto alibeba birika dogo, kulia alikamata sahani kubwa iliyokuwa na mapaja manne makubwa ya kuku waliokaangwa na mpishi stadi. Alitembea taratibu kwa madaha kama mlimbwede anayelitaka taji. Akili yangu haikufanya kazi nyingine isipokuwa kushangaa kwa uchu. Macho niliyatoa pima!
Alifika na kuweka birika na nyama juu ya meza. Nilishindwa kujizuia, nikamchombeza.
“Bibie waitwa nani? Mbona vururuvururu bila hata ya salaam!”
Maneno yangu hayakujibiwa. Aliachia tabasamu pana ambalo lilizidi kunimaliza kisha akatembea kuelekea mlango aliotumia kuingia. Sehemu za nyuma zilitikisika isivyokawaida, niligundua alifanya makusudi ili anichanganye. Masikini mateka mimi, nilitetemeka kwa uchu!
Niliishambulia nyama ya kuku na maziwa. Hakukuwa na kikombe, nilikunywa maziwa yakiwa ndani ya birika. Raha iliyoje.
Matunzo niliyopewa yalinichanganya na kunifanya nitafakari ni kwa nini nilifanyiwa vile. Kwa ujuvi nilionao, mateka wa aina yangu huteswa vilivyo kiasi cha kujuta na kutamani kufa. Kwangu ilikuwa tofauti.
Maisha yaliendelea nikiendelea kutunzwa vyema. Nilipewa vyakula vya kila aina hata nikastaajabu mambo haya. Hakika nchi hii ilikuwa ya uki na maziwa, nilinawiri matekani.
Ilikuwa asubuhi ya siku ya saba tangu niwe mateka katika nchi ya Matumbawe. Msichana anileteaye chakula aliingia. Siku zote aingiapo humsemesha asinijibu. Niliandaa kisa cha kumpima. Alipoingia nilikuwa katika kiti nimekaa. Macho yetu yalipogongana, nikatengeneza hasira bandia kisha nikanyanyuka na kujitupa kitandani. Aliweka birika la maziwa na nyama ya kuku mezani na kunifuata nilipolala.
“Una shida gani leo?” aliuliza. Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kuisikia sauti yake. Ilikuwa sauti laini nyembamba ya kike haswaa. Bila shaka sauti hii ingeweza kumtoa nyangumi baharini!
Sikumjibu, nilinyanyuka kwa hasira nikaenda kukaa katika kiti. Alinifuata na kuniuliza swali lilelile la awali. Sikumjibu. Nilinyanyuka tena nikiwa nimekunja sura na kwenda bafuni. Hakunifuata! Nilibaki bafuni kama zuzu ananyolewa ndevu!
Niliamua kurudi. Nilimkuta kakaa juu ya kiti kajiinamia kwa hudhuni. Nilimsogelea na kumuuliza tatizo. Hakunijibu, alirusha mikono na kuanza kuondoka. Nilisimama nikamkamata, haraka bila kuchelewa nikaibusu midomo yake. Alitaka kunizuia, lakini mwili haukuweza tena, alipumua kwa hisia kali na kunifanya nijipongeze kwa ushindi. Nikaongeza busu tena na tena, nikaona sasa mambo yamewiva. Nilimsogelea zaidi, hakuwa na pingamizi. Midomo yangu na yake ikakutana, bila kujitambua tukaanza kunyonyana ndimi zetu. Alihema juujuu. Nikaongeza ujuzi. Niliuruhusu mkono wangu umpapase kila mahali, nilipofanya hivyo, miguno ya kimahaba ilimtoka. Sikuwa na muda wa kupoteza. nilimbeba mzimamzima na kumbwaga kitandani. huko ningenyonya zile chuchu imara na kuchota maji kisimani.
Itaendelea Jumanne…
“Si ruhusa kuchukua hadithi hii na kuiweka katika mfumo wa sauti, kutoa kitabu, kuweka katika blogu au ‘website’ nyingine, au kufanya chochote kile bila kuwasiliana na mmiliki! Hatua kali zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayekiuka!”

Daud Makoba 0754 89 53 21

Tazama Vichekesho Vinavyotamba Katika Mtandao wa WhatsApp

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne