Kilichotokea Katika Kaburi la Mume wa Zari Kinasikitisha

Kilichotokea Katika Kaburi la Mume wa Zari Kinasikitisha
Hamu ya utajiri na imani potofu ni miongoni mwa mambo ambayo yanazidi kuichafua dunia kila uchwao. Huko Uganda, kaburi la aliyekuwa mume wa mwanadada Zari, bwana Ivan Ssemwanga limefukuliwa na wahalifu wasiojulikana.

Watu wengi wanaamini mwili wa Ivan ulizikwa ukiwa na pesa nyingi kitu ambacho huenda kikawa kimechochea ufukuaji huo. Jambo jingine linalotajwa na mashuhuda wa tukio hilo ni imani za kishirikina ambapo huenda waganga waliwatuma watu hao fuvu la Ivan.

Mara baada ya Ivan kuzikwa, waliwekwa walinzi ili kuzuia tukio kama hili. Hata hivyo, inasemekana walinzi hao waliacha kulinda baada ya kutofautiana katika gharama za malipo.

Kaburi la Ivan likiwa limefukuliwa.

Popular posts from this blog

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne