Sheikh Ponda Atii Agizo la Kamanda Mkuu wa Polisi Mambosasa

sheikh ponda na mambosasa
Siku chache zilizopita kamanda mkuu wa jeshi la polisi bwana Mambosasa alimwagiza Ponda ajisalimishe katika kituo chochote cha polisi kutokana na kauli yake iliyodaiwa kuwa ya kichochezi.
Katika kukubaliana na kauli hiyo, Ponda amewasili kituoni akiambatana na wakili wake, Abdallah Safari.
Hayo yote yamejiri baada ya mkutano aliofanya na vyombo vya habari siku ya Jumatano. Baadhi ya matamshi aliyotoa, ndiyo yanayosemwa kuwa ya kichochezi.
Hii si mara ya kwanza kwa Ponda kupewa tuhuma hizi. Mara kadhaa ametuhumiwa kwa uchochezi na hata kutupwa rumande kwa muda mrefu. Hata hivyo, katika mara zote hizo alipatikana akiwa hana hatia.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne