Mke wa Mugabe Hakamatiki, Atoa Povu Kali

Mke wa Mugabe
Kama asivyoishiwa vituko mumewe, Bi Grace Mugabe naye ni pasua kichwa! Wakati utawala wa Mugabe ukielekea ukingoni kutokana na umri mkubwa wa mzee huyo mtawala wa Zimbambwe, kumezuka hali ya kutokuaminiana hii yote ikisababishwa na watu fulani kutaka kukalia kiti cha urais baada ya Mugabe.
Bi Grace kwa kuyatambua hayo, amesema kuna uwezekano wa kutokea mapinduzi nchini humo kuhusu harakati za kumrithi Mugabe.
Grace amemshutumu bwana Mnangangwa kwa maneno makali kama alivyonukuliwa:
“Tunatishiwa usiku na mchana kwamba iwapo mtu fulani hatokuwa rais, tutauawa.”
Ugomvi wa madaraka katika nchi za Kiafrika ni suala lililozoeleka. Kupigana vikumbo, kudondoshana, kuzodoana na hata kuuana vimekuwa tabia ya wasaka madaraka. Ni wakati sasa Wazimbabwe, wanatakiwa kuungana pamoja na kutafuta muafaka mapema kabla hayajawakuta yaliyoziangusha serikali nyingi.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie