Jinsi ya Kuandika Kadi ya Mwaliko

Jinsi ya Kuandika Kadi ya Mwaliko

Kadi ya mwaliko huandikwa kwa lengo la kualika watu kuhudhuria katika sherehe fulani.
MAMBO MUHIMU KATIKA KADI YA MWALIKO
-      Jina la mhusika wa sherehe
-      Jina la anaye alikwa
-      Madhumuni ya kumwalika
-      Tarehe ya mwaliko
-      Mahali pa kukutana
-      Mahali pa kupeleka majibu kwa wasiofika
Sasa hebu tazama mfano huu kutoka swali la necta la mwaka 2009:
Katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwako, unahitaji marafiki kwa ajili ya kusherehekea siku hiyo. Andaa kadi ya mwaliko ili kuwapa taarifa rafiki zako.

Mimi Daud Makoba, ninayofuraha kukualika Bwana Kitalula Kalinga kwenye sherehe yangu ya kuzaliwa itakayofanyika siku ya tarehe 16/07/2017, saa 12.00 jioni katika ukumbi wa Godsaria hall Kimara.

Tafadhali fika na kadi hii.

Majibu kwa wasiofika
Secilia Kilongo,
S.L.P 123,
Dar es Salaam.
Simu: 0754 89 53 21.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne