WALICHOAMUA ‘WHATSAPP’ KUHUSU KUFUTA MESEJI ULIYOTUMA KWA BAHATI MBAYA
Hakuna jambo linalokosesha amani kama
kushindwa kuifuta meseji uliyoituma ‘WhatsApp’ ili watu wengine wasiweze
kuiona. Kushindwa kufuta meseji baada ya kutuma kumewahi kusababisha maafa na
mifadhaiko mikubwa sana. Mara nyingi hutokea ukadhani ujumbe ambao unaweza kuwa wa masihara au mapenzi
unatuma kwa mtu fulani lakini kwa bahati mbaya ujumbe huo ukaingia katika kundi
la watu unaoheshimiana nao sana. Aibu hii imewatesa wengi na sasa ‘WhatsApp’
wameonyesha kuguswa na jambo hili na wameamua kulitafutia ufumbuzi.
Mvujishaji wa taarifa za ‘WhatsApp,’
WABentaInfo, ametaarifu kuwa, mtandao huo kwa sasa unafanyia kazi mfumo mpya utakao
wezesha kufuta ujumbe ulioutuma kwa bahati mbaya. Tayari majaribio yameanza
kufanyika katika mifumo ya Android na iOS. Imezidi kuarifiwa mfumo huo unafanya
kazi kwa ufanisi mkubwa.
Mitandao mingine ya Telegram,
WeChat na Viber, imetumia mfumo huu kwa muda mrefu huku watumiaji wa 'WhatsApp' nao wakiomba wawekewe ‘delete for everyone.’
Huenda mfumo huu mpya ukaanza
kufanya kazi mwaka huu au mwakani. Endapo utatumika, bila shaka utapokelewa
vyema!