SERIKALI YAOMBWA KUAJIRI WAALIMU

ajira za waalimu

Huko Mwanza Serikali imetakiwa kuajiri waalimu wa kutosha ambao watasaidia vyuo mbalimbali kufikia viwango vya ufundishaji. Haya yamejiri baada ya kuwepo kwa madai ya muda mrefu katika vyuo vya mafunzo ya wauguzi na wakunga (Manesi).
Vyuo mbalimbali vya utoaji wa mafunzo haya nchini vina upungufu mkubwa wa waalimu jambo linalorudisha nyuma ufanisi na ubora wa elimu inayotolewa.
Mkurugenzi mtendaji wa chuo cha mafunzo ya uuguzi, Ndemetria Vermand alisema: “Ni kweli vyuo vyote binafsi na visivyo binafsi vina uhaba wa walimu, lakini tatizo hili ni kubwa zaidi kwa vyuo vya serikali.”
Alizidi kusisitiza hayo kuwa, utoaji wa huduma hizi utasaidia katika ubora elimu ya afya inayotolewa nchini.
Mdau mwingine wa huduma za afya, Molland Makamba alisema kuwa kuna vyuo 161 vya mafunzo ya Uuguzi na kati ya hivyo, 77 vinamilikiwa na serikali.

Hayo yote yalijiri katika hafla ya utoaji wa vyeti na tuzo kwa wafadhili watatu wa USAID ambao wamekuwa wakisaidia vyuo vya mkoani Mara na Kagera.

NA: MOWASHA| NGEME

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne