MBOWE AELEZA HALI YA TUNDU LISSU KWA SASA

HALI YA TUNDU LISSU KWA SASA

Mbunge wa Hai, Mheshimiwa Freeman  Mbowe ameeleza hali ya kiafya ya Mbunge Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi na watu wasiojulikana siku chache zilizopita.
Akiandika katika ukurasa wake wa ‘instagram’ amesema, madaktari wanatoa matumaini na ile hali ya kuhofia kupoteza maisha kwa Lissu imekwisha.
Vilevile, anazungumza na anaweza kutoa salamu. Kuhusu taarifa za maambukizi ya kifua zilizosambaa, Mbowe amekanusha na kusema taarifa hizo si za kweli.
Mwisho amewasisitiza watu wote wazidi kumuombea kila wakati aweze kupona kwa haraka na hatimaye kutoka hospitali.
Taarifa hiyo imesisitiza watu wasisikilize taarifa kutoka kwa watu wasiohusika, bali wasikilize taarifa zinazotoka kwake yeye na timu yake iliyoko Nairobi kwani wao ndiyo wapo karibu na mgonjwa.

Mbali na hayo, hii leo kumefanyika tukio la kuwasomea ‘albadri’ watu wote waliohusika na tukio la kumshambulia Tundu Lissu. Shughuli hiyo imefanyika katika mikoa kadhaa nchini.

POVU LA MWALIMU MAKOBA KWA WASANII WAVAA HOVYO

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu