Faida za Matumizi ya Alama za Kifonetiki


ALAMA ZA KIFONETIKI

Swali: kwa mifano ya kutosha, eleza jinsi wataalamu mbalimbali kama wanaleksigrofia, matabibu matamshi, wanafunzi na wanaojifunza lugha za kigeni, walimu na wanaisimu wanavyoweza kufaidika na matumizi ya alama za kifonetiki zilizowekwa na wanafonetiki?
Habwe na Karanja (2004), wanaeleza kuwa, fonetiki ni taaluma ya kisayansi inayochunguza sauti za lugha za binadamu. Wanaeleza pia, fonetiki hutimiza jukumu la kuchunguza sauti za lugha za mwanadamu zinavyotamkwa, kusafirishwa kati ya kinywa cha mnenaji na sikio la msikilizaji na jinsi zinavyofasililiwa katika ubongo wa msikilizaji.
Hyman (1975) anaeleza kuwa, fonetiki ni taaluma ambayo hususani huchunguza sauti ambazo hutumiwa na mwanadamu wakati wanapowasiliana kwa kutumia lugha.
Massamba (2004) analeza kuwa, fonetiki ni tawi la isimu linaloshughulikia uchambuzi na uchanganuzi wa sauti za lugha za binadamu, usikiaji, na utamkaji wake.
Pia wataaalamu wameeleza maana ya wanafonetiki miongoni mwao ni Habwe na Karanja (2004) wanaeleza kuwa, wanafonetiki ni wataalamu wanaojishughulisha na uchanganuzi wa jinsi sauti za lugha zinavyotamkwa, kufasiliwa kati ya kinywa cha msemaji na sikio la msikilizaji na jinsi zinavyofasiliwa katika ubongo wa msikilizaji ili kutoa ujumbe wenye maana. Wataalamu wanaeleza pia maana ya matabibu matamshi kama ifuatavyo:
Matabibu matamshi ni wataalamu ambao hujishughulisha na uchunguzi wa matatizo yanayo ambatana na utumikaji wa sauti na jinsi ya kutatua matatizo hayo. Mfano mtu akipata ajali na kuumia katika ala za sauti hujitokeza ugumu wa utamkaji katika baadhi ya maneno. Hivyo mtu huyo anaweza kusaidiwa na matabibu matamshi.
Vilevile, maana ya wanaleksigrofia inaelezwa na wataalamu kama ifuatavyo:
Mdee (1985) anaeleza kuwa, wanalesigrofia ni wataalamu wanaokusanya misamiati pamoja na tafsiri zake na kuipanga katika kitabu kiitwacho kamusi.
Kwa kutoa maana ya jumla, wanaleksigrofia ni wataalamu wanaojishughulisha na utungaji wa maneno na kuyafasiri katika kamusi.
Alama za kifonetiki ni alama ambazo hutumika katika taaluma ya fonetiki katika kumaanisha sauti za lugha fulani.
Baada ya kueleza dhana mbalimbali zinazotumika katika taaluma ya fonetiki, zifuatazo ni faida za alama za kifonetiki kwa watumiaji wa alama hizo.
Husaidia kurahisisha mawasiliano. Hii ni kutokana na ukweli kwamba watumiaji wa alama hizi wote ni watu waliobobea katika alama hizo hata katika mawasiliano yao huwa ni rahisi kuwasiliana kwa kutumia alama hizo za kifonetiki.
Mfano:
Sauti /ch/                        hutamkwa [ʧ]
Husaidia katika kutoa ajira. Kutokana na kujifunza alama mbalimbali za kifonetiki, imesaidia kuinua kiwango cha ajira kwa wataalamu wa alama hizo. Hii hutokana na sababu kwamba, wataalamu waliobobea alama hizo wanayo nafasi kubwa kuweza kuajiriwa au kujiajiri kwa kuwapa maarifa hayo watu wengine wanaohitaji kujifunza alama hizo kwa kutoa malipo kwa wataalamu wa alama hizo. Mfano kufundisha katika shule na vyuo mbalimbali.
Husaidia kujifunza lugha za kigeni. Ni dhahiri kabisa watu kuweza lugha za kigeni kupitia kujua alama za kifonetiki kwani alama zinazotumika zipo katika lugha zote duniani. Mfano: wanafunzi wazawa na hata wale wageni wanao uwezo wa kujifunza lugha tofauti na ile ya kwanza kutokana na kwamba alama hizi zitawawekea uepesi katika kujifunza lugha kwani ndizo zinazoonyesha jinsi gani neno linatakiwa kutamkwa katika umbo la ndani na umbo la nje hivyo kuchangia kujifunza lugha kiundani zaidi na hasa kwa yule anayejifunza lugha ya kigeni.
Mfano: mzungu anapojifunza lugha ya Kiswahili itamlazimu kujua jinsi maneno ya lugha anayojifunza kama Kiswahili kujua umbo la ndani na la nje kwa maneno tofauti kutoka katika lugha hiyo kwa kutumia alama za kifonetiki.
Mfano:
Umbo la ndani /nyanya/ 
Umbo la nje [ŋaŋa]]
Husaidia katika utungaji wa kamusi. Wataalamu wa alama za kifonetiki hutumia alama za kifonetiki hasa wakati wanapoyaingiza maneno katika kuandaa kamusi humsaidia kuandika maneno na jinsi yanavyotamkwa kwa kuzingatia alama za matamshi wa lugha husika. Hii itamsaidia mwandishi huyo wa kamusi kuandika maneno mengi na kuyatolea ufafanuzi wa jinsi yanavyotamkwa.
Mfano:
Neno                                                                    jinsi linavyotamkwa
Shati                                                                     [ʃati]
Chakula                                                                [ʧakula]
Husaidia kuonesha jinsi ya utamkaji wa ala mbalimbali za sauti pamoja na maneno mbalimbali. Alama mbalimbali za kifonetiki huwawezesha watumiaji wa lugha husika hata wale wanaojifunza lugha hiyo kujua jinsi maneno mbalimbali ya lugha hiyo yanavyotamkwa. Hii imesaidia watu hao kutamka maneno hayo kwa usahihi kama wazungumzaji wazawa wa lugha husika.
Licha ya kuwepo kwa faida za alama za kifonetiki, bado kuna changamoto zinazo wakabili watu wanaojifunza alama za kifonetiki kama uchache wa wataalamu. Hii hupelekea wanaojifunza alama hizo za kifonetiki kupata ugumu katika kujifunza alama hizo za kifonetiki.
Pia, uchache wa vitabu pamoja na mwongozo wa ujumla katika vitabu na alama za kifonetiki. Hii hufanya wanaojinza alama hizo za kifonetiki kutopata mwongozo sahihi wa vitabu hivyo kujikuta katika ugumu wa kujifunza. Hivyo wanaojifunza alama za kifonetiki wanatakiwa kupata miongozo sahihi ya ujifunzaji alama hizo za kifonetiki ili kurahisisha ujifunzaji wa alama hizo.

MAREJEO

Habwe na Karanja. (2004), Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi Phone Publishers
Mgullu R. (2001) Mtaala wa Isimu Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Kampala: Longhorn Publishers LTD

Massamba DPB na Wenzake. (2004), Fonolojia ya Kiswahili Sanifu (FOKISA). Dar es Salaam: TUKI

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie