Posts

Showing posts from September, 2017

Uhakiki wa Riwaya ya Vuta N’kuvute

Image
MWANDISHI: SHAFI ADAM SHAFI WACHAPISHAJI: MKUKI NA NYOTA MWAKA: 1999 MHAKIKI: MWALIMU MAKOBA Utangulizi Vuta n’kuvute ni riwaya inayozungumzia mvutano uliopo baina ya wakoloni na watawaliwa vilevile inaonyesha msuguano na mvutano uliopo kati ya wazazi na watoto katika suala la mapenzi. Maudhui DHAMIRA UKOMBOZI Mwandishi anaonyesha aina mbalimbali za ukombozi unaohitajika katika jamii. Mfano: ukombozi wa kiutamaduni. Hapa anapinga mila zinazomkandamiza mwanamke. Kwa mfano, Yasmini kulazimishwa kuolewa na Raza, ni unyanyasaji usiokubalika. Pia, ukombozi wa kisiasa. Mwandishi anaonyesha jinsi ambavyo Zanzibar ilitawaliwa na Waingereza. Wahusika Denge na wenzake wanapambana vilivyo kuhakikisha uhuru wa Zanzibar unapatikana. Ukiachilia mbali aina hizo mbili za ukombozi, mwandishi pia amejadili ukombozi wa kiuchumi na fikra. Mapenzi Mwandishi anajadili mapenzi ya kweli na yale ya uongo. Katika mapenzi ya kweli, Mwajuma, Denge na kundi lake wanamapenzi ya kweli k...

JIUNGE NA KUNDI LETU LA WHATSAPP UJIBIWE MASWALI YAKO YOTE!

Image
Jiunge katika kundi la WhatsApp la ‘ MwalimuMakoba online’ ukutane uso kwa uso na Mwalimu Makoba akiwa na wanafunzi wengine tayari kwa kuyajibu maswali yako. Kundi hili linajumuisha wanafunzi kutoka nchi nzima na hata nje ya nchi. Na linaendesha mijadala mbalimbali ambayo ni msaada mkubwa kwa wanafunzi wanaotaka kufanikiwa katika masomo. Jinsi ya kujiunga Nitumie ujumbe wowote unaoomba kuunganishwa katika kundi hili kwenye namba 0754 89 53 21. Kwa mfano: UNGA MWALIMU MAKOBA Nami nitakuunganisha mara moja. MWALIMU MAKOBA

RIWAYA| SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (22)

Image
KAMA ULIIKOSA SEHEMU ILIYOPITA ISOME HAPA: SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (21) Kisha endelea kuisoma... Mzee Samike alikuwa uvunguni. Nilistaajabu nikauliza, “umefikaje nami nimekuacha nje?” hakunijibu. Alicheka akitoka chini ya uvungu na kukaa kitandani. “Unafahamu kisa cha mimi kupelekwa jela?” aliniuliza. “Sifahamu mzee…” “Nilimfanyia mauzauza afisa mmoja wa jeshi la polisi. Kwa hasira akanitengenezea kesi bandia. Hata hivyo hawakuniweka sana wakaniachia!” “Ndiyo mzee… nilikuona gerezani nikiwa katika harakati za kukutafuta!” “Hata mimi nilikuona!” Alijibu, tukabaki tukitazamana kwa mshangao! “Chakula chako kiko sebuleni… kwa sasa nahitaji kuzungumza nawe kuhusu kuyakomesha haya mauzauza yako,” mzee alisema. Nikapata matumaini. Tulifanya mazungumzo yaliyonipa matumaini makubwa. Mzee alinambia amekwisha mzuia mtu wa ajabu na kamwe sitamuona tena. Nilifurahi nikashangilia kwa ushindi. Pia, mzee alisema hapendi kuniona nikihangaika na kazi zisizo...

VICHEKESHO HIVI KIBOKO! SOMA KWA UANGALIFU USIVUNJE MBAVU ZAKO!

Image
KAMA UNAITWA DAUDI Kama unaitwa Daudi na una demu wako amekuandikia ‘sms’ kuwa anaumwa yupo hospital anaomba umtumie hela, usimtumie maana kuna demu niko nae hapa kwenye daladala ndo kaandika hivyo na anacheka ni mzima kabisa. MAANA YA UJINGA Ujinga ni nini? Ujinga ni kulala Giza wakati bibi yako ni mwanga 😁😁 USIMWAMINI YEYOTE! Haya Maisha Duniani hupaswi kumwamini mtu yeyote.... Hivi unajua kuwa hata TANESCO wana Generator ofisini kwao.... #UaminifuUshaisha SITASAHAU Sitasahau siku nilipotoka nyumbani saa kumi na moja jioni nikiwaacha wanapeta mchele 😁😁😁😁   lakini niliporudi saa mbili nilikuta ugali mezani 😰😰😰😰 . Nilihuzunika πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜” sana na sito sahau. GAME LA NYOKA muda huu vijana walio single wamelala wameweka mikono yao  ndani ya boksa wanacheza game la nyoka.   πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ SEHEMU ZA SIRI              Sehemu za siri walikua nazo wazee Wa zamani, sisi tuna sehemu...

Uhakiki wa Riwaya ya Takadini

Image
RIWAYA: TAKADINI MWANDISHI: BEN J HANSON WACHAPISHAJI: METHEWS BOOKSTORE AND STATIONERS MWAKA: 2004 MHAKIKI: DAUD MAKOBA Muhtasari wa Riwaya Takadini ni riwaya inayojaribu kuzungumzia matatizo ya mila na desturi yaliyopo katika jamii za Kiafrika hasa sehemu za vijijini. Mwandishi anamuonyesha mhusika mkuu Takadini aliyezaliwa na ulemavu wa ngozi jinsi anavyotengwa na watoto, watu wazima na jamii yote kwa ujumla. Mwisho tunamuona Takadini akipendwa na msichana Shingai. Pamoja na vikwazo vingi, penzi la Shingai na Takadini halikufa. Baadae Shingai anapata mimba ya Takadini, kisha anajifungua mtoto asiye mlemavu. Hapo wana jamii wanashangazwa na kujikuta wakiamini kuwa hata mlemavu anaweza kuzaa mtoto asiyemlemavu. Uchambuzi wa Fani na Maudhui Maudhui Katika Riwaya ya Takadini Dhamira Ukombozi wa Kiutamaduni Utamaduni ni jumla ya maisha ya jamii. Katika jamii ya Zimbabwe watu wenye ulemavu hawakuruhusiwa kuishi, waliuawa kikatili. Ni katika jamii hii pia, watu walien...