KOLABO YA CHID BENZ NA TUPAC ILIVYOJADILIWA MITANDAONI

chid benz na tupac

Chid Benz ameamsha hisia za watu mbalimbali, maarufu na wasiomaarufu baada ya kudai amemshirikisha marehemu Tupac Shakur katika wimbo wake mpya na hivi karibuni atamleta nchini hapa ili watu wamuone.
Alizidi kueleza kuwa, Tupac hajafa bali yuko Cuba na huko ndiko alikofanikiwa kufanya naye Kolabo hiyo ya wimbo anaotarajia kuuachia.

KIKI AU MADAWA

Baada ya video hiyo kuonekana, watu mbalimbali wametoa maoni yao kuwa inawezekana amefanya hivyo akiwa na akili zake timamu kwa lengo la kupata ‘kiki.’ Wengine wametupia lawama madawa ya kulevya kwani Chid ameshindwa kabisa kuachana na matumizi ya madawa.

WALICHOANDIKA MASTAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

“Msipowapandisha hawa watu (Chid Benz na Tupac) Fiesta hatutaelewana.” Edo Kumwembe.
Naye msanii Madee aliandika msimamo wake kuwa, ndiyo sababu kubwa huwa hataki hata kuvuta sigara.

Itakumbukwa kuwa, siku chache zilizopita Chid alikamatwa kwa sakata la madawa ya kulevya na kuwekwa chini ya uangalizi mkali wa mahakama.
Unalizungumziaje hili? shusha Comment yako...

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu