ALICHOKIANDIKA MMILIKI WA MTANDAO WA FACEBOOK

mmiliki wa mtandao wa facebook


Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa mtandao wa facebook na baba wa watoto wawili aliowapata kwa mwenzi wake Priscilla Chan, amezua gumzo mtandaoni baada ya kuianika barua ambayo amemwandikia binti yake.
Katika barua hiyo, Mark amemtaka binti yake awe anatoka nje kucheza ili kuyafurahia maisha ya utoto.
Pia, amemsihi binti yake afanye mazoezi ya kukimbia kuzunguka sebule na akipenda atoke nje kucheza atakavyo.
Barua iliendelea kusema kuwa, utoto upo mara moja tu, hivyo ni busara kuufurahia na kuepuka kuwaza kupita kiasi.

GUMZO LAIBUKA MITANDAONI

Wake kwa waume wametoa maoni yao kuhusiana na barua hiyo ya Mark kwa binti yake. Wanaume wameonekana kucharuka zaidi huku wengi wao wakipanga mikakati ya kumuwinda atakapotoka ili waweze kuwa wakwe wa bilionea Mark Zuckeberg mmiliki na mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa facebook.

Unalizungumziaje hili? Shusha comment yako…

Popular posts from this blog

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne