Kiswahili Pre Necta 6
MAELEKEZO
·
Jibu maswali yote. Swali la tano ni
la lazima.
·
Fanya mtihani kwa utulivu. Mtihani
huu haupimi uwezo wako wa kupata alama nyingi bali unapima ulipo katika hatua
ya ujifunzaji ili tukusaidie kufika unapotakiwa. Ukiangalizia kwa mwenzako au
sehemu yoyote ile, utakwamisha juhudi zetu kwako.
SEHEMU A
UFAHAMU
1.
Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali.
Mzee
Bruda anaye punda wa kiume ambaye anampenda sana. Punda huyu, anamanyoya meusi
na meupe yaliyopangiliwa vyema hata humfanya aonekane mtanashati na nadhifu.
Punda
wa Bruda hula nyasi peke yake, hupenda nyasi ndefu zilizomea vyema, amalizapo
kula, hulala kwa furaha ya shibe.
Watu
wengi huenda kumtazama punda wa Bruda. Wazee hutueleza kuwa hawajapata kumuona
punda mwenye kuvutia kama yule. Hata hivyo waliomsogelea, aliwapiga mateke
wakabaki wakigugumia kwa maumivu.
Kama
nilivyosema awali kuwa, Bruda anampenda sana punda wake, punda huyu hajawahi kuadhibiwa
kwa makosa yake.
Maswali
A. Kipi kinafaa kuwa kichwa cha habari hii?
B. Ni upi ujumbe wa mwandishi wa habari hii?
C. Unafikiri ni kwa nini punda
wa Bruda alivutia sana.
D. Ama hakika anayesemwa na
mwandishi si punda bali kajificha tu katika kichaka cha fasihi pengine kwa
sababu ya uoga wake. Unadhani ni nani hasa huyu punda wa Bruda?
SEHEMU B
SARUFI
2. A. Toa maana ya sentensi kisha kwa kutumia mifano, taja aina tatu za sentensi.
B. Changanua sentensi hii kwa
njia ya matawi,
Baba analima na mama anapika.
SEHEMU C
UANDISHI
3. Andika barua ya maombi ya kazi ya ualimu katika shule ya EBENEZA SEKONDARI. Tumia ubunifu wako kutengeneza anuani na majina. Usitumie majina yako halisi.
SEHEMU D
MAENDELEO YA KISWAHILI
4. Jadili mchango wa sayansi na teknolojia katika kukuza na kueneza kiswahili. Toa hoja sita.
SEHEMU E
Fanya maswali mawili. Swali la tano ni la lazima.
FASIHI KWA UJUMLA
5. Tunga hadithi fupi kuhusu kisa chochote cha kusisimua.
6.
Kwa kutumia tamthiliya uliyosoma,
jadili wahusika wawili kwa kila kitabu huku ukitaja sifa zao.
7. Waandishi wa riwaya ni WAHENGA. Jadili.
8. Viongozi wa nchi za kiafrika ni sababu mojawapo ya kukosekana kwa maendeleo. Jadili kauli hii kwa kutumia diwani mbili ulizosoma.