Kiswahili pre NECTA 3CODE; 03, muda masaa 2;30
Jibu maswali yote;
Sehemu A (alama 10)

UFAHAMU
1.   Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata.

Huo moto utapita, mimi jivu nitabaki,
Mwanafunzi kunja ndita ,usicheke na fataki,

Nina nyota ya msumari, nawaacha na matundu,
Kibaka toa kabari, kiunoni nina mundu,

Nikinywa pombe feki, huwa siongei kiingereza,
Kama tambara la deki, kwa sakafu natereza,

Ukimheshimu kaka, ewe dada utaolewa,
Mi ndo kubwa la vibaka, nambaka hadi popobawa.

maswali

a. eleza maana ya maneno yafuatayo kama ulivyosoma kwenye shairi.
i. ndita ii.fataki iii. Mundu iv. Feki
b. ni upi ujumbe wa mwandishi wa shairi hili?
2.   Soma habari ifuatayo kisha fupisha kwa maneno yasiyozidi thelathini.
uchaguzi katika nchi za wenzetu huwa jambo la kawaida tu, hapo waweza kuona wagombea toka vyama pinzani wakipiga soga pamoja na kukumbatiana.

Mambo ni tofauti katika bara la Afrika. Anaye shinda katika uchaguzi hula, anayeshindwa hufa njaa! Hiyo humaaanisha kuwa uchaguzi ni vita!!

si rahisi kwa mtu aliyeuza shamba la urithi na nyumba pekee aliyonayo ili aweze kugombea, kukubaliana  na matokeo ya uchaguzi hata kama kashindwa kweli.

akataapo, fujo kubwa hutokea na damu nyingi humwagika!!

Mungu tuepushie balaa hili!!

SEHEMU B (alama 25)

SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA
3.   Kwa kutumia mifano, taja tofauti iliyopo baina ya mofimu huru na mofimu tegemezi.
4.   Toa maana ya vidahizo vifuatavyo kisha tunga sentensi moja kwa kila kidahizo.
i. kindakindaki ii. Kuntu iii. Jitimai iv. Jazanda v. abtali
5.   Toa maana ya sentensi kisha kwa kutumia mifano, taja aina tatu za sentensi.

SEHEMU C (alama 10)

UANDISHI
6.   Katika siku ya harusi yako. Unahitaji marafiki kwa ajili ya kusherekea. Andaa kadi ya mwaliko ili kuwataarifu rafiki zako.

SEHEMU D (alama 10)
MAENDELEO YA KISWAHILI
7.   Vyombo mbalimbali viliundwa kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili. Elezea.

SEHEMU E(alama 45)
FASIHI KWA UJUMLA
8.   Wewe ni mwanafunzi mwenye bahati ya pekee. Umeteuliwa na tume ya uchaguzi kuandika ngonjera yenye beti nne kuhusu uchaguzi mkuu 2015. Tumia bahati yako.
9.   Jadili kufaulu na kutokufaulu kimaudhui kwa waandishi wawili wa tamthiliya teule ulizosoma.
10.               Linganua mitindo iliyotumiwa na  waandishi wa diwani mbili ulizosoma.

 ORODHA YA VITABU
Ushairi
wasakatonge – M.S Khatibu
mashairi ya chekacheka – T. Mvungi
Malenga wapya – TAKILUKI

RIWAYA
watoto wa maman’tilie – E. Mbogo
Takadini – B. Hanson
Joka la mdimu – A. Safari

TAMTHILIYA
kilio chetu – Medical Aid foundation
orodha – S. Reynolds
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe – E. Semzaba

UKINGONI

“Vingi vitamu vinaua, sumu ya nini?”

mwalimu; D. Makoba.
Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne