Mtihani wa Kiswahili Kidato cha Nne | Pre Necta | Jan 2018

Mtihani wa Kiswahili Kidato cha Nne| Pre Necta| Jan 2018

JINSI YA KUUFANYA MTIHANI HUU

Mtu yeyote na kokote aliko anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba - 0754 89 53 21.
Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000 (elfu mbili) tu.
Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 na Tigo pesa 0653 25 05 66
“Kwa kuwa lengo la mtihani huu ni kutaka kujua uwezo na mapungufu ya mwanafunzi ili aweze kupewa mbinu mbadala za kumsaidia kufaulu mtihani wake wa mwisho, kuangalizia majibu hakuna faida yoyote kwani lengo la mtihani si kubaini nani atakuwa wa kwanza na yupi atakuwa wa mwisho!”
Daud Makoba – Mwalimu Makoba – Mwalimu wa Waalimu.
Unataka kufanya mtihani huu na hujaelewa taratibu zake? Wasiliana na Mwalimu Makoba kwa 0754 89 53 21.
Sasa fanya mtihani wako.
Jibu maswali yote;

SEHEMU A (alama 10)UFAHAMU

1.   Soma kifungu cha habari ifuatayo kisha jibu maswali kama ilivyoelekezwa.
Dubwana limevamia, linatafuna watoto, vijana na wazee! Meno yake ya shaba yanalifanya litoboe mpaka mifupa… wengi wameumizwa na Dubwana  hili, wengi zaidi  wanagugumia kwa maumivu.
Baada ya umasikini na ujinga, ndipo hufuata Dubwana hili hatari, dude ambalo limepotosha maadili na kuifanya heshima ya jamii yetu izorote!
Ajabu ya yote, washenga wa Dubwana ndio haohao wanaojinasibu katika majukwaa ya kanyaga tunese, kuwa wataliondoa Dubwana na kulitupilia mbali! Uliona wapi pepo akamfukuza pepo?
Yangu macho!!

MASWALI

i. Andika kichwa cha habari hiyo kwa maneno yasiyopungua matano.

ii.  Kwa mujibu wa habari uliyosoma unahisi Dubwana ni nini? 

iii. Ni watu wa aina gani wanatafunwa na Dubwana hili? 

iv. Ni akina nani wanajinasibu kuwa wataliondoa Dubwana?

v. Ni yapi maoni yako kuhusu washenga wa Dubwana?


2.   Soma kifungu cha habari ifuatayo kisha fupisha kwa maneno yasiyozidi ishirini.

Baada ya kuachana na mke wangu Nyangema, aliniachia mtoto mdogo wa miezi minne tu. Kama ujuavyo mimi ni mtu wa shughuli hivyo nisingeweza kulea mtoto Yule peke yangu, niliamua kutafuta dada wa kazi za ndani. Nikampata dada “mashallah”, mwenye guu kama chaki mwendo wa tembo na macho katikati kama anayesinzia – jina lake aliitwa Shushu.

Lakini sasa nasikitika kukuta  barua mezani na mtoto wangu akilia hovyo, barua yenyewe inasema Shushu anakwenda kijijini kwao kugombea Ubunge! Ajabu kwelikweli ati mfanya kazi wangu wa ndani naye kaamua kujiajiri katika sekta hii rasmi. Akipita nitakuwa nikimuita mheshimiwa Shushu! Ajabu kwelikweli!

Sasa tujiandae kuona  maji yakipanda mlima!

Shushu mfanya kazi wangu wa ndani anautaka  ubunge!

SEHEMU B Sarufi na Matumizi ya  Lugha (alama 25)

3.   Katika kila moja ya sentensi zifuatazo, onesha kosa moja la kisarufi kisha andika sentensi hiyo kwa usahihi.
a.   Kinyonga kinakimbia.
b.   Arusi ya dada yenu zitakuwa Disemba 2015.
c.   Mwaka huu jua zinachoma sana.
d.   Tafadhali nikope shilingi mia nitakurudishia keshokutwa.
e.   Kichumba hiki kichafu sana.

4.   Onyesha dhima ya kiambishi “ni” kilichopigiwa msitari katika sentensi zifuatazo.
a.  Alinisaidia
b. Wajumbe wapo mkutanoni
c. Wakubalieni
d.  Yeye ni mvivu
e.  Nina kalamu

SEHEMU C (Alama 10) UTUNGAJI

5. Andika insha yenye maneno mia moja kuhusu mada hii.
“kampeni za uchaguzi mkuu 2015”.

SEHEMU D (alama 10) HISTORIA YA LUGHA

6.   “Kiswahili ni kibantu”. Thibitisha kauli hii kwa kutumia hoja sita.

SEHEMU E (alama 45)

chagua maswali matatu, swali la 10 ni la lazima.

7.   “Mwandishi wa fasihi ni mchunguzi wa jamii ambaye huyaweka wazi maovu mbalimbali”. Jadili jinsi kazi za washairi wawili kati ya hao walioorodheshwa zilivyosadifu kauli hii.

8.   “Matendo yasiyo na utu hujadiliwa na wasanii”. Thibitisha kauli hii kwa kutumia riwaya mbili kati ya hizo zilizoorodheshwa.
9. "Tamthiliya huacha mafunzo makubwa kwa hadhira waitazamapo ikiwa jukwaani." jadili kauli hiyo kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma.
10. Tunga shairi la kimapokeo lenye beti nne, ukiusifia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

ORODHA YA VITABU

Ushairi
wasakatonge – M.S Khatibu
mashairi ya chekacheka – T. Mvungi
Malenga wapya – TAKILUKI

RIWAYA
watoto wa maman’tilie – E. Mbogo
Takadini – B. Hanson
Joka la mdimu – A. Safari

TAMTHILIYA
kilio chetu – Medical Aid foundation
orodha – S. Reynolds
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe – E. Semzaba

Ukingoni.

Mwalimu Makoba

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu