Jaribio la Kiswahili Kidato cha Tatu

kompyuta katika giza

MUDA SAA 1
MAELEKEZO;
JIBU MASWALI YOTE
VIFAA VISIVYOHUSIANA NA SHERIA ZA MTIHANI HAVIRUHUSIWI
SEHEMU A.
1.   Chagua jibu sahihi
i.             Ni ipi maana ya fasihi andishi
a.   Ni sanaa ambayo hutumia maneno yaliyoandikwa ili kufikisha ujumbe
b.   Ni sanaa ya uandishi
c.   Ni sanaa muhimu inayohusika na uandishi mbalimbali
ii.            Hadithi inaweza kugawanywa katika tanzu mbili ambazo ni
a.   Lakabu na majazi
b.   Hadithi fupi na ushairi
c.   Hadithi fupi na riwaya
SEHEMU B
2.   Andika K kwa jibu la kweli na S kwa jibu lisilo la kweli
i.             Kuna mikondo sita ya hadithi
ii.            Wahusika wachache ni jambo mojawapo la kuzingatia katika utungaji wa hadithi fupi
SEHEMU C
3.   Tunga hadithi fupi kuhusu kisa chochote cha kusisimua
4.   Tunga tamthiliya fupi isiyozidi kurasa moja kuhusu ajira kwa watoto.MAJIBU YA JARIBIO LA KWANZA
SEHEMU A (20%)
1.   i. A
ii. C
SEHEMU B (20%)
2.   i. S
ii. K
SEHEMU C (60%)
3.   hadithi iwe na sifa zote za hadithi fupi kama vile;
*Wahusika wachache
*Mandhari finyu
*Fupi
     4.   Tamthiliya iwe na sifa zote za tamthiliya kama vile;
          *Matumizi ya dayolojia

          *Wahusika wachache n.k


Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne