Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi
Kitaalamu Zaidi, Naweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi Kwa Tsh. 8,000/= tu. Barua Tsh. 3,000/= na CV Tsh. 5,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nami. Umewekeza katika elimu yako, una kila sifa ya kupata kazi fulani lakini hupati kazi hiyo, inawezekana kabisa sababu mojawapo inayokufanya usipate kazi unayoitaka ni kutokujua kuandika barua ya maombi ya kazi. Kwa muda mrefu nimekuwa nikiulizwa na wanafunzi na wasomaji wa mtandao wangu kuhusu jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi kwa kiswahili, na wengine huuliza kuhusu jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi kwa kiingereza. Wengine huomba kazi serikalini, wengine kazi za udereva, ualimu, udaktari na wengine kazi za uhudumu wa baa. Kazi zote siku hizi zinahitaji kuandika barua, hata kama unataka kujitolea, lazima utaandika barua! Bahati mbaya ni kuwa, hata mtandaoni mifano inayooneshwa kuwa ni ya barua za maombi ya kazi mingi yake siyo sahihi, kila mmoja ana njia zake. Ni kama mashetani kil