Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie
MWANDISHI: EMMANUEL MBOGO WACHAPISHAJI: HEKO PUBLISHERS MWAKA: 2002 MHAKIKI: MWALIMU MAKOBA Wasifu wa Mwandishi Emmanuel Mbogo ni Profesa wa drama na fasihi na amehudumu katika vyuo vikuu mbalimbali ikiwemo, Chuo Kikuu cha Kenyatta Kenya na Chuo Kikuu Huria. Mbogo ni mwanafasihi mahiri sana katika Afrika ya Mashariki. Muhtasari wa Riwaya Maman’tilie, mama mwenye watoto wawili lakini wote wamefukuzwa shule kwa kukosa ada na sare. Anajitahidi hapa na pale ili apate, lakini wapi? Pesa imegeuka nyoka inateleza kwenye nyasi. Mumewe Mzee Lomolomo hana muda, yeye kila kukuchapo huelekea bunge la walevi kunywa pombe tani yake. Akiwa huko hunywa na kurudi nyumbani akiwa mbwii! Mwisho mwandishi anauliza swali gumu, ‘Nani anajali?’ Uchambuzi wa Fani na Maudhui Maudhui Katika Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie Maudhui hujumuisha mawazo na pengine mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma mtunzi ama mwandishi wa kazi ya fasihi akaandika kazi yake. Dhamira Dhamira ni lile wazo linalom...