SAFARI YA KUUSAKA MWEZI (sehemu ya tatu)
Minza alitusalimu, kisha akakaa pembeni, sikutaka kupoteza Muda niliingia ndani ya Mapandagila 214, tayari kwa safari ya kuusaka mwezi. Nilikaa ndani ya Mapandagila 214, nikaiwasha, ikaunguruma kama simba, nilitaka kuwaonesha kuwa mimi ni mtaalamu wa kuendesha Mapandagila ndani na nje ya nchi ya Lahaja. Taratibu nikairusha hewani, niliizungusha polepole katika uwanja ule wa nyumba ya mfalme, nikakunja kona na kuirusharusha kama mpira, halafu nikaitembeza kwa mwendo wa konakona mithili ya kiluwiluwi ndani ya maji, hapo nikaona mfalme na watu wake wakinipigia makofi. Sikutaka kulewa sifa, nikapiga gia kubwa, Mapandagila ikapaa juu, hapo nikatuma taarifa makao makuu, “Mapandagila inatembea mwendo wa sauti tisa za kunguru dume!” Chombo kilikimbia kwa mwendo wa kasi mpaka kikaitoka Dunia. Nikasikia katika mtambo wangu wa mawasiliano watu wa makao makuu wakinipongeza kwa hatua hiyo. Nikatabasamu kwa ushindi md...